Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waraka kwa Waebrania 6:9-12

Waraka kwa Waebrania 6:9-12 SRUV

Lakini, wapenzi, ijapokuwa twanena hayo, kuhusu habari zenu tumeamini mambo yaliyo mazuri zaidi, na yaliyo na wokovu. Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia. Nasi twataka sana kila mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hata mwisho; ili msiwe wavivu, bali mkawe kama hao wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Waraka kwa Waebrania 6:9-12