Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Habakuki 1:1-5

Habakuki 1:1-5 SRUV

Ufunuo aliouona nabii Habakuki. Ee BWANA, nilie hadi lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa. Mbona wanionesha uovu, na kunifanya nione mabaya? Maana uharibifu na udhalimu u mbele yangu; kuna ugomvi, na mashindano yatokea. Kwa sababu hiyo sheria imelegea, wala hukumu haipatikani; kwa maana watu wabaya huwazunguka wenye haki; kwa sababu hiyo hukumu inayotolewa huwa imepotoshwa. Angalieni, enyi mlio kati ya mataifa, katazameni, kastaajabuni sana; kwa maana mimi natenda tendo siku zenu, ambalo hamtaliamini hata mkiambiwa.

Soma Habakuki 1