Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 27

27
Isaka ambariki Yakobo
1 # Mwa 48:10; 1 Sam 3:2; Mhu 12:3 Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa. 2#Mit 27:1; Yak 4:14 Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu. 3#Mwa 25:27,28 Basi, nakuomba, chukua uta wako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo; 4#Mwa 48:9,15; 49:28; Kum 33:1; Ebr 11:20 ukaniandalie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa.
5Na Rebeka akasikia, Isaka aliposema na Esau mwanawe. Basi Esau akaenda mbugani awinde mawindo, ayalete. 6Rebeka akamwambia Yakobo mwanawe, akisema, Angalia, nimemsikia baba yako akisema na Esau, ndugu yako, akinena, 7Niletee mawindo, ukanifanyie chakula kitamu ili nile, na kukubariki mbele za BWANA kabla ya kufa kwangu. 8#Mwa 27:13 Basi, mwanangu, sikiliza sauti yangu kama nitakavyokuagiza. 9Nenda sasa kundini ukanitwalie wana-mbuzi wawili walio wema, nami nitawafanya chakula kitamu kwa baba yako, namna ile aipendayo. 10#Mwa 48:15 Kisha utampelekea baba yako, apate kula, ili akubariki kabla ya kufa kwake.
11 # Mwa 25:25 Yakobo akamwambia Rebeka mamaye, Esau ndugu yangu ni mtu mwenye malaika, na mimi ni mtu laini. 12#Mwa 27:22; 9:25; Kum 27:18 Labda baba yangu atanipapasa, nami nitakuwa machoni pake kama mdanganyifu; nami nitaleta juu yangu laana wala si baraka. 13#Mwa 43:9; 1 Sam 25:24; 2 Sam 14:9; Mt 27:25 Mamaye akamwambia, Laana yako na iwe juu yangu, mwanangu, usikie sauti yangu tu, nenda ukaniletee wana-mbuzi. 14#Mwa 27:4,9 Akaenda, akawatwaa, akamletea mamaye. Mamaye akafanya chakula kitamu namna ile aliyopenda babaye. 15#Mwa 27:27 Kisha Rebeka akatwaa mavazi mazuri ya Esau mwanawe mkubwa, aliyokuwa nayo nyumbani, akamvika Yakobo mwanawe mdogo. 16Na ngozi za wana-mbuzi akamvika mikononi, na katika ulaini wa shingo yake. 17Naye akampa Yakobo mwanawe mikononi mwake hicho chakula kitamu, na mkate aliouandaa.
18Akaja kwa baba yake, akasema, Babangu. Akasema, Mimi hapa, U nani wewe, mwanangu? 19#1 Fal 13:18; 14:2; Isa 28:15; Zek 13:4 Yakobo akamwambia babaye, Mimi ni Esau, mzaliwa wako wa kwanza, nimefanya kama ulivyoniambia. Inuka, tafadhali, ukae kitako, ule mawindo yangu, ili roho yako inibariki. 20#Kut 20:7 Isaka akamwuliza mwanawe, Imekuwaje umepata upesi namna hii, mwanangu? Akasema, Kwa sababu BWANA, Mungu wako, amenifanikisha. 21#Mwa 27:12 Isaka akamwambia Yakobo, Karibu, tafadhali, ili nikupapase, mwanangu, nione kwamba wewe ndiwe mwanangu Esau, ama siyo. 22Basi Yakobo akamkaribia Isaka, babaye, naye akampapasa, akasema, Sauti ni sauti ya Yakobo, lakini mikono ni mikono ya Esau. 23#Mwa 27:16 Wala hakumtambua, kwa maana mikono yake ilikuwa kama mikono ya Esau, ndugu yake, yenye malaika; basi akambariki. 24#Rum 3:7,8; Efe 4:25 Akamwuliza, Wewe ndiwe kweli mwanangu Esau? Akasema, Ndimi. 25Akasema, Niletee karibu nami nipate kula mawindo ya mwanangu, ili roho yangu ikubariki. Akamsogezea karibu, naye akala; kisha akamletea mvinyo, akanywa. 26Isaka, baba yake, akamwambia, Njoo karibu sasa, ukanibusu, mwanangu. 27#Hos 14:6; Wim 2:13; Ebr 6:7 Akakaribia akambusu. Naye akasikia harufu ya mavazi yake, akambariki akasema,
Tazama, harufu ya mwanangu
Ni kama harufu ya shamba alilolibariki Bwana.
28 # Ebr 11:20; Kum 33:13,28; 2 Sam 1:21; Hes 18:12; Zab 65:9; Zek 9:17 Mungu na akupe ya umande wa mbingu,
Na manono ya nchi,
Na wingi wa nafaka na mvinyo.
29 # Mwa 9:25; 12:3; 49:8; Hes 24:9 Mataifa na wakutumikie
Na makabila wakusujudie,
Uwe bwana wa ndugu zako,
Na wana wa mama yako na wakusujudie.
Alaaniwe yeyote yule atakayekulaani,
Na abarikiwe yeyote yule atakayekubariki.
Esau aomba baraka
30Ikawa Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo, na punde tu baada ya Yakobo kutoka mbele ya Isaka, babake, mara Esau ndugu yake akaja kutoka katika kuwinda kwake. 31#Mwa 27:4 Naye pia amefanya chakula kitamu akamletea babaye, akamwambia baba yake. Babangu na ainuke, ale mawindo ya mwanawe, ili uweze kunibariki. 32Isaka, baba yake, akamwuliza, U nani wewe? Akasema, Mimi ni mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza. 33#Mwa 28:3,4; Hes 23:20; Efe 1:3; Rum 11:29 Isaka akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema, Ni nani basi yule aliyetwaa mawindo akaniletea? Nami nimekwisha kula kabla hujaja wewe, nikambariki; naam, naye atabarikiwa.
34 # Ebr 12:17 Esau aliposikia maneno ya babaye, akalia kilio kikuu na chenye uchungu mwingi sana, akamwambia babaye, Nibariki na mimi, mimi nami, Ee babangu. 35#1 The 4:6 Akasema, Nduguyo amekuja kwa hila, akaichukua baraka yako. 36#Mwa 25:29-34 Akasema, Je! Hakuitwa Yakobo kwa haki, maana amejitia mahali pangu mara mbili hizi? Alichukua haki yangu ya mzaliwa wa kwanza, na sasa ameichukua baraka yangu. Akasema, Je! Hukuniwekea na mimi mbaraka?
37 # 2 Sam 8:14 Isaka akajibu, akamwambia Esau, Tazama, nimemfanya awe bwana wako, na ndugu zake wote nimempa kuwa watumishi wake; kwa nafaka na mvinyo nimemtegemeza, nami nikufanyie nini sasa, mwanangu? 38#Ebr 12:17 Esau akamwambia babaye, Una mbaraka mmoja tu, babangu? Unibariki mimi, mimi nami, Ee babangu. Esau akapaza sauti yake, akalia.
39 # Ebr 11:20 Isaka, baba yake, akajibu, akamwambia,
Angalia, penye manono ya nchi patakuwa makao yako,
Na penye umande wa mbingu unaotoka juu.#Ebr 11:20
40 # Mwa 25:23; 36:8; 2 Fal 8:20; 2 Sam 8:14; Oba 1:18-20 Kwa upanga wako wewe utaishi, nawe utamtumikia nduguyo;
Na itakuwa utakapoponyoka,
Utalivunja kongwa lake katika shingo yako.
Yakobo akwepa ghadhabu ya Esau
41 # Mwa 37:4; 50:3; Oba 1:10; 1 Yoh 3:12 Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ile baraka babaye aliyombariki. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo. 42#Zab 64:5 Rebeka akaarifiwa maneno ya Esau, mwanawe mkubwa. Akatuma mtu kumwita Yakobo, mwanawe mdogo, akamwambia, Tazama, katika habari zake Esau, ndugu yako, anajifariji moyo wake, maana anakusudia kukuua. 43#Mwa 11:31 Na sasa, mwanangu, sikia sauti yangu, uondoke, ukimbilie kwa Labani, ndugu yangu huko Harani; 44ukae kwake siku chache, hadi ghadhabu ya ndugu yako iishe; 45hadi ikuondokee ghadhabu ya ndugu yako, akasahau uliyomtenda. Ndipo nitakapotuma watu kukuchukua kutoka huko. Kwa nini nifiwe nanyi nyote wawili siku moja?
46 # Mwa 24:3; 26:35; 28:8 Rebeka akamwambia Isaka, Rohoni mwangu sina raha kwa sababu ya hao binti za Hethi. Kama Yakobo akitwaa mke katika binti za Hethi, kama hawa binti za nchi, maisha yangu yatanifaidi nini?

Iliyochaguliwa sasa

Mwanzo 27: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha