Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 22

22
Amri ya kumtoa Isaka kafara
1 # Ebr 11:17-19; Yak 1:12-14 Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Abrahamu, akamwambia, Ee Abrahamu! Naye akasema, Mimi hapa. 2#2 Nya 3:1; Yn 3:16 Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia. 3#Ebr 11:17-19 Abrahamu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu. 4Siku ya tatu Abrahamu akainua macho yake, akapaona mahali pakiwa bado ni mbali. 5Abrahamu akawaambia vijana wake, Kaeni ninyi hapa pamoja na punda, na mimi na kijana tutakwenda kule, tukaabudu, na kuwarudia tena. 6#Yn 19:17; 1 Pet 2:24 Basi Abrahamu akazitwaa kuni za hiyo sadaka, akamtwika Isaka mwanawe; akatwaa moto na kisu mkononi mwake, wakaenda wote wawili pamoja. 7Isaka akasema na Abrahamu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa? 8#1 Pet 1:19 Abrahamu akasema, Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, mwanangu. Basi wakaendelea wote wawili pamoja. 9#Yak 2:21; Yn 10:17,18; Ebr 11:17 Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu, Abrahamu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni. 10#Isa 53:6-12 Abrahamu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe. 11Ndipo malaika wa BWANA akamwita kutoka mbinguni, akasema, Abrahamu! Abrahamu! Naye akasema, Mimi hapa. 12#1 Sam 15:22; Mwa 26:5; Rum 8:32; Yak 2:22 Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, kwa kuwa hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee. 13#1 Kor 5:7,8 Abrahamu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo dume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Abrahamu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. 14Abrahamu akapaita mahali hapo Yehova-yire,#22:14 Yehova-yire: maana yake ni BWANA atapata. kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana.#22:14 ‘atatoa’.
15Malaika wa BWANA akamwita Abrahamu mara ya pili kutoka mbinguni 16#Ebr 6:13-14; Zab 105:9; Lk 1:73 akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, 17#Ebr 11:12; Mwa 15:5; Yer 33:22; Mwa 13:16; 24:60; Mik 1:9 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki lango la adui zao; 18#Mdo 3:25; Mwa 12:3; 18:18; Gal 3:8,9,16,18; Mwa 22:3,10; 26:5 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu. 19Basi Abrahamu akawarudia vijana wake, wakaondoka, wakaenda zao pamoja mpaka Beer-sheba; Abrahamu akakaa huko Beer-sheba.
Wana wa Nahori
20 # Mwa 11:29 Ikawa baada ya mambo hayo, Abrahamu akaambiwa ya kwamba, Tazama, Milka naye amemzalia Nahori ndugu yako wana; 21#Ayu 1:1; 32:2 Usi, mzaliwa wa kwanza wake, na Buzi nduguye, na Kemueli, baba wa Aramu; 22na Kesedi, na Hazo, na Pildashi, na Yidlafu, na Bethueli. 23#Mwa 24:15 Bethueli akamzaa Rebeka; hao wanane Milka alimzalia Nahori ndugu wa Abrahamu. 24Na suria wake Reuma naye alizaa Teba na Gahamu na Tahashi na Maaka.

Iliyochaguliwa sasa

Mwanzo 22: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha