Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 18:1-8

Mwanzo 18:1-8 SRUV

BWANA akamtokea Abrahamu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa joto. Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka chini, akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako. Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu. Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, kwa maana mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema. Basi Abrahamu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Tayarisha haraka vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye mikate. Abrahamu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng'ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akaharakisha kuiandaa. Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandalia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala.

Soma Mwanzo 18

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mwanzo 18:1-8