Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wagalatia 6

6
Chukulianeni mizigo
1 # Mt 18:15; Yak 5:19 Ndugu zangu, mtu akishikwa katika kosa lolote, ninyi mlio wa Roho mrejesheni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. 2Mchukuliane mizigo na hivyo kuitimiza sheria ya Kristo. 3Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake. 4#2 Kor 13:5 Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. 5#Rum 14:12 Maana kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe.
6 # 1 Kor 9:14 Mwanafunzi na amshirikishe mwalimu wake katika mema yote. 7Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. 8#Rum 8:13; Yn 6:63; 3:6 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. 9#2 The 3:13 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. 10#2 Pet 1:7 Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.
Mawaidha ya mwisho na baraka
11Tazameni niandikavyo kwa herufi kubwa niwaandikiapo kwa mkono wangu mimi mwenyewe! 12#Gal 5:11; Flp 3:18 Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili, ndio wanaowashurutisha kutahiriwa; makusudi wasiudhiwe kwa ajili ya msalaba wa Kristo, hilo tu. 13Kwa maana hata wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria; bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kuona fahari katika miili yenu. 14#1 Kor 1:31; 2:2 Lakini mimi, la hasha, nisione fahari juu ya kitu chochote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulubishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu. 15#Gal 5:6; 1 Kor 7:19 Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutotahiriwa, ila kiumbe kipya. 16#Zab 125:5; 128:6; Flp 3:3 Na wote watakaoenenda kwa kanuni hiyo, amani na iwe kwao na rehema, naam, kwa Israeli wa Mungu.
17 # 2 Kor 4:10 Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.
18Ndugu zangu, neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu. Amina.

Iliyochaguliwa sasa

Wagalatia 6: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha