Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 35:4-21

Kutoka 35:4-21 SRUV

Kisha Musa akanena na mkutano wote wa wana wa Israeli, akawaambia, Neno hili ndilo aliloliamuru BWANA, akisema, Katwaeni kati yenu matoleo kwa BWANA; mtu yeyote aliye na moyo wa kupenda, ayalete matoleo; dhahabu na fedha na shaba; na nyuzi za rangi ya buluu, zambarau, nyekundu, na kitani nzuri, na singa za mbuzi; na ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, ngozi za pomboo na mbao za mshita; na mafuta kwa hiyo taa, na viungo vya manukato kwa hayo mafuta ya kutiwa, na kwa huo uvumba mzuri; na vito vya shohamu, vito vya kutiwa kwa hiyo naivera na kwa hicho kifuko cha kifuani. Na kila mtu kati yenu aliye na moyo wa hekima na aje, na kuyafanya hayo yote ambayo BWANA ameyaagiza; yaani, hiyo maskani na hema yake, kifuniko chake, vifungo vyake, mbao zake, mataruma yake, viguzo vyake na vitako vyake; hilo sanduku, miti yake, hicho kiti cha rehema na lile pazia la sitara; na hiyo meza, miti yake, vyombo vyake vyote na hiyo mikate ya wonyesho; na hicho kinara cha taa kwa mwanga, vyombo vyake, taa zake na hayo mafuta kwa nuru; na hiyo madhabahu ya kufukizia uvumba, miti yake, hayo mafuta ya kupaka, huo uvumba mzuri na hicho kisitiri cha mlango, mlangoni mwa hiyo maskani; na hiyo madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, pamoja na wavu wake wa shaba, miti yake, vyombo vyake vyote hilo birika na kitako chake; na hizo kuta za nguo za ua, viguzo vyake, vitako vyake na pazia la lango la ua; na vile vigingi vya maskani, vigingi vya ua na kamba zake na mavazi yenye kufumwa kwa uzuri, kwa ajili ya kutumika ndani ya mahali patakatifu, hayo mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika kazi ya ukuhani. Basi mkutano wote wa wana wa Israeli wakaondoka hapo mbele ya Musa. Wakaja kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye roho yake ilimfanya kuwa apenda, nao wakaleta sadaka za kumpa BWANA, kwa kazi ya hema ya kukutania, na kwa utumishi wake, na kwa hayo mavazi matakatifu.

Soma Kutoka 35

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Kutoka 35:4-21

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha