Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 32

32
Sanamu ya ndama ya dhahabu
1 # Mdo 7:40; Kut 24:18; Kum 9:9; Isa 41:6,7 Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata. 2#Amu 8:24 Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mniletee. 3Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletea Haruni. 4#1 Fal 12:28; Mdo 7:41; Kut 20:23; Kum 9:16; Amu 7:3,4; Neh 9:18; Zab 106:19; Isa 46:6; Rum 1:23 Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha; nao wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri. 5#Law 23:2; 2 Fal 10:20 Naye Haruni alipoona jambo hili, akajenga madhabahu mbele yake; Haruni akatangaza akasema, Kesho itakuwa sikukuu kwa BWANA. 6#1 Kor 10:7 Wakaondoka asubuhi na mapema, wakatoa dhabihu, wakaleta sadaka za amani, watu wakaketi kula na kunywa, wakaondoka wacheze.
7 # Kum 9:12; Mwa 6:11; Kum 4:16; 32:5; Amu 2:19; Hos 9:9 BWANA akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao, 8#Kut 20:3,4,23; Kum 9:16; 1 Fal 12:28 wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu wakasema, “Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri”. 9#Kut 33:3; 34:9; Kum 9:6; 31:27; 2 Nya 30:8; Isa 48:4; Mdo 7:51 Tena BWANA akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, ni watu wakaidi#32:9 Katika Kiebrania ni ‘shingo ngumu’. 10#Kum 9:14; Hes 14:12 basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu. 11#Hes 14:13-19; Kum 9:18,26-29; Zab 74:1; 106:23 Musa akamsihi sana BWANA, Mungu wake, na kusema, BWANA, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu? 12Kwa nini Wamisri waseme, kuwa “Amewatoa ili awatende mabaya, apate kuwaua milimani na kuwaangamiza watoke juu ya uso wa nchi?” Geuza katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako. 13#Mwa 22:16-17; 12:7; 13:15; 35:12; 17:8; Ebr 6:13 Mkumbuke Abrahamu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele. 14#Hes 23:19; Kum 32:36; 2 Sam 24:16; 1 Nya 21:15; Yer 18:8; Hos 11:8; Yoe 2:13; Yn 3:10 Na BWANA akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu wake.
15 # Kum 9:15 Basi, Musa akageuka akashuka katika mlima, na zile mbao mbili za mawe mikononi mwake; mbao zilizoandikwa pande zote mbili, upande huu na upande huu ziliandikwa. 16#Kut 31:18 Na zile mbao zilikuwa kazi ya Mungu nayo maandiko yalikuwa maandiko ya Mungu, yaliyochorwa katika zile mbao. 17Na Yoshua aliposikia kelele za watu walipokuwa wakipiga kelele, akamwambia Musa, Kuna kelele ya vita kambini. 18Akasema, Hiyo si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushinda vitani, wala si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushindwa; bali kelele za watu waimbao ndizo ninazozisikia mimi. 19Hata alipokaribia kambini akaiona ile ndama, na ile michezo. Hasira ya Musa ikawaka, akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini ya mlima. 20Akaitwaa ile ndama waliyoifanya, akaichoma moto, akaisaga hata ikawa mavumbi, akainyunyiza juu ya maji, akawanywesha wana wa Israeli. 21#Mwa 20:9 Musa akamwambia Haruni Watu hawa wamekufanya nini hata ukaleta dhambi hii kuu juu yao? 22#Kut 15:24 Haruni akasema, Hasira ya bwana wangu isiwake, wewe unawajua watu hawa, ya kuwa wamejielekeza kwa mabaya. 23Maana waliniambia, Katufanyie miungu, itakayokwenda mbele yetu, kwa maana mtu huyo Musa, aliyetutoa katika nchi ya Misri, hatujui yaliyompata. 24Nikawaambia, Mtu yeyote aliye na dhahabu na aivunje; basi wakanipa, nami nikaitupa ndani ya moto, akatoka ndama huyu.
25 # Kut 33:4,5; 2 Nya 28:19 Basi Musa alipoona ya kuwa watu hawa wameasi, maana Haruni amewaacha waasi, na kuwa dhihaka kati ya adui zao, 26ndipo Musa akasimama katika mlango wa kambi, akasema, Mtu yeyote aliye upande wa BWANA, na aje kwangu. Wana wa Lawi wote wakamkusanyikia 27#Kum 33:9; Hes 25:11; Kum 13:6; Zek 13:3 Akawaambia, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kila mtu na ajifunge upanga wake pajani mwake, akapite huku na huko toka mlango hata mlango kati kambi, mkamchinje kila mtu ndugu yake, na kila mtu mwenziwe na kila mtu jirani yake. 28Na hao wana wa Lawi wakafanya kama vile alivyosema Musa, wakaanguka siku ile kama watu elfu tatu. 29Musa akasema, Jiwekeni wakfu kwa BWANA leo,#32:29 Katika Kiebrania yaweza kuwa, ‘mmewekwa wakfu leo, au leo mmejiweka wakfu wenyewe’. kila mtu juu ya mwanawe na juu ya ndugu yake; ili awape baraka leo. 30#1 Sam 12:20; 2 Sam 16:12; Amo 5:15 Hata asubuhi yake Musa akawaambia watu, Mmetenda dhambi kuu; na sasa nitakwenda juu kwa BWANA, labda nitafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi yenu. 31Musa akarejea kwa BWANA akasema, Aa! Watu hawa wametenda dhambi kuu wamejifanyia miungu ya dhahabu. 32#Zab 69:29; Ufu 3:5; 22:19; Kum 9:14; Rum 9:3; Zab 56:8; 139:16; Flp 4:3 Lakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao – na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika. 33#Law 23:30; Eze 18:4 BWANA akamwambia Musa, Mtu yeyote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu. 34#Hes 20:16; Amo 3:14; Rum 2:5,6 Basi sasa uende ukawaongoze watu hawa mpaka mahali pale ambapo nimekwambia habari zake; tazama, malaika wangu atakutangulia; pamoja na hayo siku nitakayowajia nitawapatiliza kwa ajili ya dhambi yao. 35#2 Sam 12:9 BWANA akawapiga hao watu, kwa tauni kwa kuifanya ile ndama, ambayo Haruni aliifanya.

Iliyochaguliwa sasa

Kutoka 32: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia