Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 27

27
Madhabahu ya sadaka za kuchomwa
1 # Kut 38:1; Eze 43:13 Nawe fanya madhabahu ya mti wa mshita; urefu wake utakuwa ni dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano; hiyo madhabahu itakuwa mraba; na kwenda juu kwake kutakuwa dhiraa tatu. 2#1 Fal 1:50; 2:28; Zab 128:2; Hes 16:38 Nawe fanya pembe nne katika pembe zake nne; hizo pembe zitakuwa za kitu kimoja na madhabahu; nawe utayafunika shaba. 3#1 Sam 2:13,14 Na vyombo vyake vya kuyaondoa majivu yake utavifanya, na majembe yake, na mabakuli yake, na uma zake, na meko yake; vyombo vyake vyote utavifanya vya shaba. 4Nawe uifanyie hiyo madhabahu wavu wa shaba; kisha utie pete nne za shaba katika hizo pembe nne za ule wavu. 5Nawe tia huo wavu chini ya kizingo kiizungukacho madhabahu upande wa chini, ili huo wavu ufikie katikati ya hiyo madhabahu. 6Nawe fanya miti kwa ajili ya madhabahu, miti ya mshita, na kuifunika shaba. 7#Hes 4:15; Isa 52:11 Na hiyo miti itatiwa katika pete, na ile miti itakuwa katika pande mbili za madhabahu, wakati wa kuichukua. 8#Kut 25:40; 26:30; Ebr 8:5; Mdo 7:44 Uifanye ya mbao, yenye mvungu ndani yake; kama ulivyooneshwa mlimani, ndivyo watakavyoifanya.
Uwanja na mapambo yake
9 # Kut 38:9; Zab 100:4 Nawe fanya ua wa maskani; upande wa kusini wa kuelekea kusini kutakuwa na chandarua ya nguo ya kitani nzuri yenye kusokotwa, kwa huo ua, urefu wake upande mmoja utakuwa ni dhiraa mia moja; 10na nguzo zake zitakuwa nguzo ishirini, na vitako vyake ishirini, vitako vyake vitakuwa vya shaba; kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha. 11Ni vivyo hivyo upande wa kaskazini, urefu wake hiyo chandarua utakuwa ni dhiraa mia moja, na nguzo zake ishirini, na vitako vyake ishirini vitakuwa vya shaba; kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha. 12Na upande wa magharibi, upana wa ua kutakuwa na chandarua ya dhiraa hamsini; nguzo zake kumi, na vitako vyake kumi. 13Na upana wa ule ua upande wa mashariki kuelekea mashariki utakuwa ni dhiraa hamsini. 14Chandarua upande mmoja wa lango itakuwa dhiraa kumi na tano upana wake; nguzo zake zitakuwa tatu na vitako vyake vitatu. 15Upande wa pili ni vivyo hivyo chandarua ya dhiraa kumi na tano; nguzo zake tatu, na vitako vyake vitatu. 16Na kwa lile lango la ua patakuwa na kisitiri cha dhiraa ishirini, kitakuwa cha nguo ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshonaji taraza; nguzo zake zitakuwa nne, na vitako vyake vinne. 17Nguzo zote za ule ua ziuzungukao pande zote zitakuwa na vitanzi vya fedha; kulabu zake za fedha, na vitako vyake vya shaba. 18Urefu wa huo ua utakuwa dhiraa mia moja, na upana wake utakuwa dhiraa hamsini kotekote, na kwenda juu kwake dhiraa tano; yawe ya nguo ya kitani nzuri, na vitako vyake vitakuwa vya shaba. 19Vyombo vyote vya maskani vitumiwavyo katika utumishi wake wote, na vigingi vyake vyote, na vigingi vyote vya ule ua, vitakuwa vya shaba.
Mafuta kwa ajili ya taa
20 # Law 24:2 Nawe waamuru wana wa Israeli wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya nuru, ili kufanya ile taa kuwaka daima. 21#Kut 25:16; Kut 30:8; 1 Sam 3:3; 2 Nya 13:11; Kut 28:43; 29:9; Law 3:17; 16:34 Ndani ya ile hema ya kukutania, nje ya hilo pazia, lililo mbele ya huo ushuhuda, Haruni na wanawe wataitengeza tangu jioni hadi asubuhi mbele ya BWANA; itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyao vyote kwa ajili ya wana wa Israeli.

Iliyochaguliwa sasa

Kutoka 27: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia