Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 17

17
Maji toka mwambani
1 # Hes 20:2-13; Kut 16:1; 19:2; Hes 33:12,14 Mkutano wote wa wana wa Israeli ukasafiri, kutoka bara ya Sini kwa safari zao, kama BWANA alivyowaagiza, wakatua Refidimu; napo hapakuwa na maji, watu wanywe. 2#Hes 20:3; Kum 6:16; Zab 78:41; Isa 7:12; Mt 4:7; 1 Kor 10:9 Kwa hiyo hao watu wakamgombeza Musa, wakasema, Tupe maji tunywe. Musa akawaambia, Kwa nini mnanigombeza? Mbona mnamjaribu BWANA? 3#Kut 16:2 Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung'unikia Musa, wakasema, Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu? 4#1 Sam 30:6; Yn 8:59; 10:31 Musa akamlilia BWANA, akisema, Niwatendee nini watu hawa? Bado kidogo nao watanipiga kwa mawe. 5#Eze 2:6; Hes 20:8 BWANA akamwambia Musa, Pita mbele ya watu, ukawachukue baadhi ya wazee wa Israeli pamoja nawe; na ile fimbo yako ambayo uliupiga mto kwayo, uitwae mkononi mwako, ukaende. 6#Zab 105:41; 114:8; 1 Kor 10:4 Tazama, nitasimama mbele yako huko, juu ya lile jabali katika Horebu; nawe utalipiga jabali, na maji yatatoka, watu wapate kunywa. Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli. 7#Zab 95:8; Ebr 3:8 Akapaita mahali pale jina lake Masa,#17:7 Katika Kiebrania ni ‘jaribu’. na Meriba#17:7 Katika Kiebrania ni ‘kunung'unika’. kwa sababu ya ugomvi wa wana wa Israeli, na kwa sababu walimjaribu BWANA, wakisema, Je! BWANA yu kati yetu au sivyo?
Waamaleki Washindwa na Waisraeli
8 # Mwa 36:12; Hes 24:20; Kum 25:17; 1 Sam 15:2 Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu. 9#Mdo 7:45; Ebr 4:8 Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, uende ukapigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. 10Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima. 11#Yak 5:16 Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda. 12Lakini mikono ya Musa ililegea; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitengemaza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa. 13Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga. 14#Kum 25:17-19; 1 Sam 15:2-9; Kut 34:27; 1 Sam 30:1; 2 Sam 8:12; Ezr 9:14 BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu. 15#Amu 6:24 Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yahweh-nisi;#17:15 Maana yake ni Bwana wangu au Mungu wangu ni Bendera yangu. 16akasema, BWANA ameapa;#17:16 Maana katika Kiebrania si dhahiri. BWANA atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi.

Iliyochaguliwa sasa

Kutoka 17: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia