Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Esta 4

4
Esta Akubali Kuwasaidia Wayahudi
1 # 2 Sam 1:11; Ayu 1:20; Mdo 14:14; Yos 7:6; Eze 27:30; Mwa 27:34 Basi Mordekai alipojua mambo yote yaliyofanyika, alizirarua nguo zake, akajivika gunia na kujipaka majivu, akatoka hadi katikati ya mji, akalia kwa sauti kuu ya uchungu. 2Pia akafika hata mbele ya mlango wa mfalme; maana hakuna awezaye kuingia ndani ya mlango wa mfalme akiwa amevaa magunia. 3Na katika kila mkoa, ambako amri ya mfalme na mbiu yake imewasili, palikuwako msiba mkuu kwa Wayahudi, na kufunga, na kulia, na kuomboleza; hata na wengi wakalala juu ya gunia na majivu. 4Basi wajakazi wake Esta, na wasimamizi wake wa nyumba, wakamjia, wakampasha habari; naye malkia akahuzunika mno; akampelekea Mordekai mavazi, ili kumvika, na kumwondolea gunia lake; lakini yeye hakukubali.
5Kisha Esta akamwita Hathaki, towashi mmojawapo wa mfalme, aliyemwagiza amhudumue Esta, akamtuma kwa Mordekai, ili ajue mambo hayo, na maana yake ni nini. 6Basi yule Hathaki akatoka nje kumwendea Mordekai kwenye uwanda wa mji ulipo mbele ya mlango wa mfalme. 7#Est 3:9 Naye Mordekai akamweleza yote yaliyompata, na hesabu ya fedha Hamani aliahidi kulipa katika hazina ya mfalme, ili Wayahudi waangamizwe. 8#Est 3:14,15; Ayu 9:15; Mit 15:1; Mdo 12:20 Pia akampa na nakala ya andiko la mbiu ya kuwaangamiza, iliyotangazwa Shushani, ili amwoneshe Esta, na kumweleza; tena amwagize aingie kwa mfalme, kumsihi na kuwaombea watu wake.
9Basi Hathaki akaja, akamwambia Esta maneno ya Mordekai. 10Ndipo Esta akasema na Hathaki, akamtuma tena kwa Mordekai, kusema, 11#Est 5:1,2; 8:4; Dan 2:9 Watumishi wote wa mfalme wanajua sana, hata na watu wa majimbo ya mfalme, ya kwamba mtu yeyote, akiwa mwanamume au mwanamke, atakayemjia mfalme katika ua wa ndani, wala hakuitwa, kuna sheria moja kwake, ni kwamba auawe; isipokuwa yeye ambaye mfalme atamnyoshea fimbo ya dhahabu, ili aishi; wala mimi sikuitwa niingie kwa mfalme yapata siku thelathini.
12Basi wakamwambia Mordekai maneno ya Esta. 13#Mit 29:25 Naye Mordekai akawaagiza wampelekee Esta jibu la kusema, Wewe usijidhanie kuwa wewe utaokoka nyumbani mwa mfalme, zaidi ya Wayahudi wote. 14#Law 26:42; Hes 23:22-24; Yer 30:10; Amo 9:8; Zab 75:5,6; Mhu 3:1; Isa 14:27; 54:17; Yer 30:10,24; Dan 4:17,35 Kwa maana wewe ukinyamaza kabisa wakati huu, ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada na wokovu kwa njia nyingine; ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako; lakini ni nani ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huu? 15Basi Esta akawatuma ili wamjibu Mordekai, 16#Yoe 1:14; Yon 3:4; Zab 34:22; Mit 29:25 Nenda ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Susa, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie. 17Basi Mordekai akaenda zake, akafanya yote kama vile Esta alivyomwagiza.

Iliyochaguliwa sasa

Esta 4: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha