Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waefeso 6:2-7

Waefeso 6:2-7 SRUV

Waheshimu baba yako na mama yako; hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri na kuishi siku nyingi katika dunia. Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana. Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba mnamtii Kristo; wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekazao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo; kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu

Soma Waefeso 6