Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Amosi 7

7
Nzige, moto na timazi
1Haya ndiyo aliyonionesha Bwana MUNGU; tazama, aliumba nzige mwanzo wa kuchipuka kwake mimea wakati wa vuli; na tazama, ilikuwa mimea ya wakati wa vuli baada ya mavuno ya mfalme. 2Ikawa, nzige walipokwisha kula majani ya nchi, ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, samehe, nakusihi; Yakobo atasimamaje? Kwa maana ni mdogo. 3#Kum 32:36; Zab 106:45; 1 Nya 21:15; Hos 11:8; Yoe 2:14; Yon 3:10; Yak 5:16 BWANA akaghairi katika jambo hili. Jambo hili halitakuwa, asema BWANA.
4Haya ndiyo aliyonionesha Bwana MUNGU; tazama, Bwana MUNGU aliita ili kushindana kwa moto; nao ukaviteketeza vilindi vikuu, ukataka kuiteketeza nchi kavu. 5Ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, acha, nakusihi; Yakobo atasimamaje? Kwa maana ni mdogo. 6#Zab 102:17 BWANA akaghairi katika jambo hili pia. Jambo hili halitakuwa, asema Bwana MUNGU.
7Haya ndiyo aliyonionesha; na tazama, Bwana alisimama karibu na ukuta uliojengwa kwa timazi, mwenye timazi mkononi mwake. 8#2 Fal 21:13; Isa 28:17; Mik 7:18 BWANA akaniambia, Amosi, unaona nini? Nikasema, Naona timazi. Ndipo Bwana akasema, Tazama, nitaweka timazi kati ya watu wangu Israeli; sitawapita tena kamwe; 9#Mwa 26:23; 2 Fal 15:10 na mahali palipoinuka pa Isaka patakuwa ukiwa, na mahali patakatifu pa Israeli pataharibika; nami nitaondoka nishindane na nyumba ya Yeroboamu kwa upanga.
Amazia amlalamikia mfalme
10 # 1 Fal 12:32; 2 Fal 14:23 Ndipo Amazia, kuhani wa Betheli, akapeleka habari kwa Yeroboamu, mfalme wa Israeli, akisema, Amosi amefanya fitina juu yako kati ya nyumba ya Israeli; nchi haiwezi kustahimili maneno yake yote. 11Kwa maana Amosi asema hivi, Yeroboamu atakufa kwa upanga, na bila shaka Israeli atapelekwa uhamishoni, mbali na nchi yake. 12Tena Amazia akamwambia Amosi, Ewe mwonaji, nenda zako, ikimbilie nchi ya Yuda, ukale mkate huko, ukatabiri huko; 13#Amo 2:12 lakini usitabiri tena huku Betheli; kwa maana ni mahali patakatifu pa mfalme, nayo ni nyumba ya kifalme. 14#2 Fal 2:5; Zek 13:5 Ndipo Amosi akajibu akamwambia Amazia, Mimi sikuwa nabii, wala sikuwa mwana wa nabii; bali nilikuwa mchungaji, na mtunza mikuyu; 15naye BWANA akanitwaa, katika kufuatana na kundi; BWANA akaniambia, Nenda uwatabirie watu wangu Israeli. 16#Isa 30:10; Mik 2:6 Basi, sasa lisikie neno la BWANA; Wewe unasema, Usitabiri juu ya Israeli, wala usitoe neno lako juu ya nyumba ya Isaka; 17#Yer 28:12; 29:21; Omb 5:11 kwa hiyo, BWANA asema hivi, Mke wako atakuwa kahaba mjini, na wana wako na binti zako wataanguka kwa upanga, na shamba lako litagawanywa kwa kamba; na wewe mwenyewe utakufa katika nchi iliyo najisi; na bila shaka Israeli atapelekwa uhamishoni mbali na nchi yake.

Iliyochaguliwa sasa

Amosi 7: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha