Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Amosi 2

2
1 # Isa 15:1—16:14; 25:10-12; Yer 48:1-47; Eze 25:8-11 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Moabu, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu aliichoma moto mifupa ya mfalme wa Edomu hata ikawa chokaa; Sef 2:8-11; 2 Fal 3:27 2#Yer 48:41 lakini nitatuma moto juu ya Moabu, nao utayateketeza majumba ya Keriothi; na Moabu atakufa pamoja na mshindo, na kelele, na sauti ya tarumbeta; 3#Hes 24:17; Yer 48:7 nami nitamkatilia mbali mwamuzi atoke kati yake, nami nitawaua wakuu wake pamoja naye, asema BWANA.
Hukumu kwa Yuda
4 # Law 26:14; 2 Sam 12:9,10; 2 Nya 36:14-17; Neh 1:7; Isa 5:24; 28:15; Eze 20:13,16; Dan 9:11; Yer 16:19 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Yuda, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA; wala hawakuzishika amri zake; na maneno yao ya uongo yamewakosesha, ambayo baba zao waliyafuata; 5#Hos 8:14 lakini nitatuma moto juu ya Yuda, nao utayateketeza majumba ya Yerusalemu. Hukumu kwa Israeli.
6 # Isa 29:21; Amo 5:11,12 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Israeli, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wamewauza wenye haki kwa fedha, na maskini kwa jozi ya viatu; 7#Isa 10:2; Eze 22:11; Law 20:3; Eze 36:20; Rum 2:24 nao hukanyaga vichwa vya maskini katika mavumbi ya nchi na kuwasukuma walioteseka kutoka kwa njia yao; na mtu na baba yake wanamwendea mwanamke mmoja, na kulitia unajisi jina langu takatifu; 8#Kut 22:26; 1 Kor 10:21 nao hujilaza karibu na kila madhabahu juu ya nguo zilizowekwa rehani, na katika nyumba ya Mungu wao hunywa divai ya watu waliotozwa fedha. 9#Hes 21:24; Kum 3:8-11 Lakini nilimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini niliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini. 10Pia niliwapandisha ninyi kutoka nchi ya Misri, nikawaongoza muda wa miaka arubaini jangwani, ili mpate kuimiliki nchi ya Mwamori. 11#Amu 13:5; Hes 6:1-8 Nami nikawainua watu miongoni mwa wana wenu wawe manabii, na katika vijana wenu wawe Wanadhiri; je! Sivyo hivyo, enyi wana wa Israeli? Asema BWANA. 12#Isa 30:10; Mdo 4:18 Lakini mliwapa Wanadhiri mvinyo wanywe; mkawaamuru manabii, mkisema, Msifanye unabii.
13Tazameni, nitawalemea ninyi,
Kama gari lilemeavyo lililojaa miganda.
14Naye apigaye mbio atapotewa na kimbilio;
Wala aliye hodari hataongeza nguvu zake;
Wala shujaa hatajiokoa nafsi yake;
15Wala apindaye upinde hatasimama;
Wala aliye mwepesi wa miguu hataokoka;
Wala apandaye farasi hatajiokoa nafsi yake;
16Naye mwenye moyo mkuu miongoni mwa mashujaa
Atakimbia uchi siku ile, asema BWANA.

Iliyochaguliwa sasa

Amosi 2: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia