Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo 18:24-28

Matendo 18:24-28 SRUV

Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzaliwa wa Aleksandria, msemaji mzuri, akafika Efeso; naye alikuwa na ujuzi wa Maandiko. Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa bidii habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu. Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Priskila na Akila walipomsikia wakampeleka kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi. Na alipotaka kuvuka bahari aende mpaka Akaya, ndugu wakamhimiza, wakawaandikia wale wanafunzi wamkaribishe, naye alipofika akawasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa neema ya Mungu. Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akionesha kwa maneno ya Maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo.

Soma Matendo 18

Video for Matendo 18:24-28

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Matendo 18:24-28