Matendo 16:16-18
Matendo 16:16-18 SRUV
Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, tulikutana na kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi, aliyewapatia bwana zake faida kubwa kwa kuagua. Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu. Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.