Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Samweli 13

13
Amnoni na Tamari
1 # 2 Sam 3:2,3; 1 Nya 3:2,9 Ikawa baada ya hayo, Absalomu, mwana wa Daudi, alikuwa na dada yake mzuri, aliyeitwa Tamari, naye Amnoni, mwana wa Daudi, akampenda. 2Akasononeka Amnoni, hata akaugua, kwa ajili ya yule dada yake Tamari, maana huyu msichana alikuwa mwanamwali, Amnoni akaona ni vigumu kumtendea neno lolote. 3#1 Sam 16:9; 1 Nya 2:13 Lakini Amnoni alikuwa na rafiki, jina lake Yonadabu, mwana wa Shama, nduguye Daudi; naye Yonadabu alikuwa mtu mwerevu sana. 4#Isa 3:9; Eze 23:16 Naye akamwambia, Kwa nini, Ee mwana wa mfalme, unakonda hivi siku kwa siku? Hutaki kuniambia? Amnoni akamwambia, Nampenda Tamari, dada ya kaka yangu, Absalomu. 5Yonadabu akamwambia, Lala kitandani mwako ujifanye mgonjwa na babako atakapokuja kukutazama, umwambie, Mwache ndugu yangu, Tamari, aje, nakusihi, anipe mkate nile, akaandae chakula machoni pangu nikione, nikakile mkononi mwake. 6#Mwa 18:6 Basi Amnoni akalala, akajifanya mgonjwa; na mfalme alipokuja kumtazama, Amnoni akamwambia mfalme, Mwache ndugu yangu, Tamari, aje, nakusihi, aniandalie mikate miwili machoni pangu, nipate kula mkononi mwake. 7Basi Daudi akatuma mjumbe aende nyumbani kwa Tamari, akasema, Nenda sasa nyumbani kwa Amnoni, ndugu yako, ukamwandalie chakula. 8Akaenda Tamari nyumbani kwa nduguye Amnoni; naye alikuwa amelala. Akachukua unga, akaukanda, akaiandaa mikate machoni pake, akaioka mikate. 9#Mwa 45:1; Amu 3:19; Yn 3:20 Akalitwaa kaango, akaisongeza mbele yake; lakini alikataa kula. Naye Amnoni akasema, Toeni watu wote kwangu. Ndipo watu wote wakaondoka. 10Amnoni akamwambia Tamari, Kilete chakula chumbani, nipate kula mkononi mwako. Basi Tamari akaitwaa mikate aliyoiandaa, akamletea Amnoni nduguye mle chumbani. 11#Mwa 39:12; Mit 7:13; Mhu 7:26 Naye alipokwisha kuileta karibu naye, ili ale, Amnoni akamkamata, akamwambia, Njoo ulale nami, dada yangu. 12#Law 18:9,11; 20:17; Mwa 34:7; Amu 19:23; 20:6; Mit 7:7-23 Naye akamjibu, La, sivyo, ndugu yangu, usinilazimishe; kwani haifai kutendeka hivi katika Israeli; usitende upumbavu huu. 13#Mwa 19:8; Law 18:9,11; Amu 19:24 Nami nichukue wapi aibu yangu? Wewe nawe utakuwa kama mmoja wa wapumbavu wa Israeli. Basi, sasa, nakusihi, useme na mfalme; kwa maana hatakukataza kunioa. 14#Law 18:9; 20:17; Kum 22:25; 27:22; Amu 20:5; 2 Sam 12:11 Lakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamlazimisha, akalala naye. 15Kisha Amnoni akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako. 16Naye akamwambia, Sivyo, kwa kuwa mabaya haya ya kunifukuza ni makuu kuliko yale uliyonitendea. Lakini alikataa kumsikiliza. 17Ndipo akamwita mtumishi wake aliyemtumikia, akasema, Mtoe sasa mwanamke huyu kwangu, ukafunge mlango nyuma yake. 18#Mwa 37:3; Amu 5:30; Zab 45:14 Naye alikuwa amevaa kanzu ndefu; kwa kuwa kwa nguo hizo huvikwa binti za mfalme waliokuwa wanawali. Ndipo mtumishi wake akamtoa nje, akafunga mlango nyuma yake. 19#Yos 7:6; 2 Sam 1:2; Ayu 2:12; 42:6; Yer 2:37 Naye Tamari akatia majivu kichwani mwake, akairarua hiyo kanzu ndefu yake aliyoivaa, akaweka mkono kichwani akaenda zake huku akilia kwa sauti. 20Huyo Absalomu nduguye akamwambia, je! Amekuwa nawe Amnoni nduguyo? Ila sasa tulia, dada; ni nduguyo; usilitie moyoni jambo hili. Basi Tamari akakaa hali ya ukiwa nyumbani mwa nduguye Absalomu. 21Na mfalme Daudi alipoyasikia maneno hayo yote, alikasirika sana. 22#Law 19:17; Mit 10:18; 1 Yoh 2:9,11; Efe 4:26,31 Ila Absalomu hakusema na Amnoni wala kwa heri wala kwa shari; kwa maana Absalomu alimchukia Amnoni kwa kumlazimisha dada yake Tamari.
Absalomu ajilipiza kisasi juu ya dadaye
23 # Mwa 38:12; 1 Sam 25:4; 2 Fal 3:4; Yos 17:18; Amu 7:24 Ikawa baada ya miaka miwili mizima, Absalomu alikuwa na wenye kukata manyoya ya kondoo huko Baal-hasori uliopo upande wa Efraimu; naye Absalomu akawaalika wana wote wa mfalme. 24Absalomu akamjia mfalme, akasema, Tazama sasa, mimi mtumishi wako ninao wakata manyoya ya kondoo; basi mfalme na aende, nakusihi, na watumishi wake pamoja nami mtumishi wako. 25Mfalme akamwambia Absalomu, Sivyo, mwanangu, tusiende sote, tusije tukakulemea. Akamsihi sana; asikubali kwenda, ila akambariki. 26Ndipo akasema Absalomu, Kama huji, nakusihi, mwache ndugu yangu Amnoni aende nasi. 27Mfalme akamwambia, Kwa nini aende nawe? Lakini Absalomu akamsihi sana, naye akamwacha Amnoni na wana wote wa mfalme waende naye. 28#Mwa 9:21; 19:32-35; Amu 19:6; Rut 3:7; 1 Sam 25:36; Est 1:10; Zab 104:15 Kisha Absalomu akawaamuru watumishi wake, akasema, Angalieni basi, moyo wake Amnoni utakapofurahiwa kwa mvinyo; nami nitakapowaambia, Mpigeni Amnoni, kisha mwueni, msiogope; si mimi niliyewaamuru? Iweni hodari, na wenye ujasiri. 29Basi watumishi wa Absalomu wakamfanyia Amnoni kama alivyoamuru Absalomu. Ndipo wakaondoka wana wote wa mfalme, wakapanda kila mtu nyumbu wake, wakakimbia. 30Ikawa, walipokuwa njiani, habari zikamfikia Daudi, kusema, Absalomu amewaua wana wote wa mfalme, wala hata mmoja wao hakusalia. 31#Mwa 37:29,34; 2 Sam 1:11; 12:16 Ndipo mfalme akainuka, akararua nguo zake, akalala chini; nao watumishi wake wote wakasimama karibu naye, nguo zao zikiwa zimeraruliwa. 32Akajibu Yonadabu, mwana wa Shama, nduguye Daudi, akasema, Asidhani bwana wangu ya kwamba wamewaua vijana wote, wana wa mfalme; maana ni Amnoni peke yake aliyekufa; yakini haya yamekusudiwa kwa kinywa chake Absalomu tangu siku ile alipomshika kwa nguvu dada yake, Tamari. 33#2 Sam 19:19 Basi sasa bwana wangu mfalme asilitie neno hili moyoni, kudhani ya kwamba wana wote wa mfalme wamekufa maana ni Amnoni peke yake aliyekufa. 34Lakini Absalomu akakimbia. Na kijana yule aliyekuwa mlinzi akainua macho yake, akaona, na tazama, kuna watu wengi wanakuja kwa njia ya upande wa kilima nyuma yake. 35Ndipo Yonadabu akamwambia mfalme, Tazama, wana wa mfalme wamekuja; kama mimi mtumishi wako nilivyosema, ndivyo ilivyo. 36Ikawa alipokwisha kusema, tazama, wana wa mfalme walikuja, nao wakapaza sauti zao wakalia; mfalme naye akalia, na watumishi wake wote, kilio kikubwa mno. 37#2 Sam 3:3; 1 Nya 3:2 Lakini Absalomu akakimbia, akamwendea Talmai, mwana wa Amihudi, mfalme wa Geshuri. Naye Daudi akamlilia mwanawe kila siku.
38 # 2 Sam 14:23; 15:8 Basi Absalomu akakimbia, akaenda Geshuri, akakaa huko muda wa miaka mitatu. 39#Mwa 38:12 Mfalme Daudi akatamani kutoka kumwendea Absalomu kwa kuwa ametulizwa kwa habari ya Amnoni, kwa maana amekufa.

Iliyochaguliwa sasa

2 Samweli 13: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia