Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Wafalme 25

25
Kuanguka na kuchukuliwa mateka kwa Yuda
1 # 2 Nya 36:17; Yer 34:2; 39:1; Eze 24:1 Ikawa katika mwaka wa tisa wa kutawala kwake, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya mwezi huo, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, akaja, yeye na jeshi lake lote, kupigana na Yerusalemu, akapanga hema zake kuukabili; nao wakajenga ngome juu yake pande zote. 2Basi mji huo ulihusuriwa hata mwaka wa kumi na moja wa mfalme Sedekia. 3Siku ya tisa ya mwezi wa nne njaa ilikuwa nzito ndani ya mji, hata hapakuwa na chakula kwa watu wa nchi. 4#Yer 39:4; 52:7; Eze 12:12 Ndipo mahali pakabomolewa katika ukuta wa mji, watu wote wa vita wakakimbia usiku kwa njia ya lango lililokuwa kati ya zile kuta mbili, karibu na bustani ya mfalme; (basi wale Wakaldayo walikuwa wakiuzuia mji pande zote;) mfalme akaenda kwa njia ya Araba. 5Lakini jeshi la Wakaldayo wakamfuatia mfalme, wakampata katika nchi tambarare ya Yeriko; na jeshi lake lote walikuwa wametawanyika na kumwacha. 6#2 Fal 23:33 Ndipo wakamkamata mfalme, wakamchukua kwa mfalme wa Babeli huko Ribla; wakatoa hukumu juu yake. 7#Yer 39:7; Eze 12:13 Wakawaua wana wa Sedekia mbele ya macho yake, wakampofusha macho Sedekia, wakamfunga kwa pingu, wakamchukua mpaka Babeli.
8 # 2 Fal 24:12 Hata mwezi wa tano, siku ya saba ya mwezi, ndio mwaka wa kumi na tisa wa mfalme Nebukadneza, mfalme wa Babeli, Nebuzaradani, kamanda wa askari walinzi, mtumishi wa mfalme wa Babeli, akaingia Yerusalemu. 9#2 Nya 36:19; Zab 74:3-7; 79:1; Isa 64:11; Yer 7:14; Mik 3:12; Amo 2:5 Akaiteketeza nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme; na nyumba zote za Yerusalemu, naam, kila nyumba kubwa aliiteketeza kwa moto. 10#Neh 1:3 Na jeshi lote la Wakaldayo, waliokuwa pamoja na huyo kamanda wa askari walinzi, wakazibomoa kuta za Yerusalemu pande zote. 11#Yer 39:9; 52:15 Na mabaki ya watu waliosalia katika mji, nao wale walioasi, na kumkimbilia mfalme wa Babeli, na mabaki ya watu wote wengine, watu hao Nebuzaradani, kamanda wa askari walinzi, akawachukua mateka. 12#2 Fal 24:14; Yer 40:7 Lakini huyo kamanda wa askari walinzi akawaacha watu walio maskini ili wawe watunza mizabibu na wakulima.
13 # 2 Fal 20:17; 1 Fal 7:15 Na zile nguzo za shaba zilizokuwako nyumbani mwa BWANA, na vitako, na ile bahari ya shaba, iliyokuwamo nyumbani mwa BWANA, Wakaldayo wakavivunja vipande vipande, wakaichukua shaba yake yote mpaka Babeli. 14#Kut 27:3; 1 Fal 7:45,50 Nayo masufuria, na majembe, na makasi, na miiko, na vyombo vyote vya shaba walivyokuwa wakivitumia, wakavichukua vyote. 15#Kut 37:23; 2 Nya 24:14; Est 1:9-11; Dan 5:2 Na vyetezo, na mabakuli; vilivyokuwa vya dhahabu katika dhahabu, na vilivyokuwa vya fedha katika fedha, kamanda wa askari walinzi akavichukua. 16Zile nguzo mbili, na ile bahari moja, na vile vitako, Sulemani alivyoifanyia nyumba ya BWANA; shaba ya vyombo hivyo vyote haikuwa na uzani. 17Urefu wa nguzo moja ulikuwa dhiraa kumi na nane, na kichwa cha shaba kilikuwa juu yake; na urefu wa kichwa ulikuwa dhiraa tatu; na mapambo ya wavu na makomamanga juu ya kichwa hicho kotekote, yote yalikuwa ya shaba. Nayo nguzo ya pili ilikuwa vivyo hivyo, pamoja na ule wavu.
18 # Yer 52:24; 1 Nya 6:14; Ezr 7:1; Yer 21:1; 29:25,29 Na kamanda wa askari walinzi akamtwaa Seraya, kuhani mkuu, na Sefania, kuhani wa pili, na wale walinzi watu wa mlango; 19#Yer 52:25 na katika mji akamtwaa towashi mmoja, aliyewasimamia watu wa vita; na watu watano katika wale waliosimama mbele ya mfalme, walioonekana mjini; na katibu wa jemadari wa jeshi, aliyewaandika watu wa nchi; na watu sitini katika watu wa nchi, walioonekana mjini. 20Kisha Nebuzaradani, kamanda wa askari walinzi, akawatwaa hao, akawaleta kwa mfalme wa Babeli huko Ribla. 21#Law 26:33; Kum 4:26; 28:36,64; 2 Fal 17:20; 23:27; Yer 24:9,10; 25:9; Amo 5:27 Naye mfalme wa Babeli akawapiga, na kuwaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Hivyo Yuda wakachukuliwa utumwani kutoka nchi yao.
Gedalia afanywa gavana wa Yuda
22 # Yer 40:5 Na kwa habari ya watu waliosalia katika nchi ya Yuda, aliowasaza Nebukadneza, mfalme wa Babeli, akamweka Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani awe mtawala juu yao.
23Kisha, wakuu wote wa majeshi, wao na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemweka Gedalia kuwa mtawala, wakamwendea Gedalia huko Mispa; nao ni hawa, Ishmaeli mwana wa Nethania, na Yohana mwana wa Karea, na Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofa, na Yezania mwana wa Mmaaka, wao na watu wao. 24#Yer 27:12; 38:17 Na Gedalia akawaapia wao na watu wao, akawaambia, Msiogope kwa ajili ya watumishi wa Wakaldayo; kaeni katika nchi; mkamtumikie mfalme wa Babeli; itakuwa vyema kwenu. 25#Yer 41:1,2; Zek 7:5; 8:19 Lakini ikawa katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania, mwana wa Elishama, mmoja wa wazao wa kifalme, na watu kumi pamoja naye, wakamwendea Gedalia, wakampiga hata akafa, na hao Wayahudi na Wakaldayo waliokuwa pamoja naye huko Mispa. 26#Yer 41:16-18; 42:14-22; 43:4,7 Wakaondoka watu wote, wadogo kwa wakubwa, pamoja na wakuu wa majeshi, wakainuka kwenda Misri; kwa kuwa waliwaogopa Wakaldayo.
Yekonia aachiliwa kutoka gerezani
27 # Kum 28:68; Yer 41:17; 52:31; Mwa 40:13,20 Ikawa katika mwaka wa thelathini na saba wa kuhamishwa kwake Yekonia,#25:27 Au, Yehoyakini. mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, Evil-merodaki, mfalme wa Babeli, katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake, akamwinua kichwa Yekonia, mfalme wa Yuda, akamtoa gerezani. 28#Yer 27:6-11; Est 4:4; 8:15; Dan 2:37; 5:18,19 Akasema naye maneno mazuri, akaweka kiti chake cha enzi juu ya viti vya enzi vya wafalme waliokuwa pamoja naye huko Babeli; 29#Mwa 41:14; 2 Sam 9:7 naye akambadilishia mavazi yake ya gerezani, akala chakula mbele yake daima, siku zote za maisha yake. 30Na kwa posho yake, alipewa posho ya daima na mfalme, siku kwa siku sehemu, siku zote za maisha yake.

Iliyochaguliwa sasa

2 Wafalme 25: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia