Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Wafalme 13

13
Yehoahazi atawala Israeli
1Katika mwaka wa ishirini na tatu wa Yoashi mwana wa Ahazia, mfalme wa Yuda, Yehoahazi mwana wa Yehu alianza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; akatawala miaka kumi na saba. 2Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, akayafuata makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli; wala hakuyaacha. 3#Law 26:17; Kum 4:23,24; 6:13; Amu 2:14; Zab 7:11; Isa 10:5,6; 42:8; Nah 1:3,6; 2 Fal 8:12 Hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, akawatia mkononi mwa Hazaeli mfalme wa Shamu, na mkononi mwa Ben-hadadi mwana wa Hazaeli, siku zote. 4#Hes 21:7; Amu 6:6-8; Zab 78:34; 106:23; Yer 2:27; Kut 3:7; 2 Fal 14:26; Mit 15:3; Yer 32:19 Naye Yehoahazi akamsihi BWANA, BWANA akamsikiliza; kwa kuwa aliyaona mateso ya Israeli, jinsi mfalme wa Shamu alivyowatesa. 5#2 Fal 14:25,27; Lk 2:11 (BWANA akawapa Israeli mwokozi, nao wakatoka mikononi mwa Washami; wana wa Israeli wakakaa hemani mwao kama zamani za kwanza. 6#1 Fal 16:33 Lakini hawakuyaacha makosa ya nyumba ya Yeroboamu, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli, lakini wakaendelea katika hayo; nayo ile Ashera ikakaa katika Samaria). 7#Amo 1:3 Kwa kuwa hakumwachia Yehoahazi watu ila wapandao farasi hamsini, na magari kumi, na askari elfu kumi waendao kwa miguu; kwa kuwa mfalme wa Shamu aliwaharibu, akawaponda mfano wa mavumbi yaliyokanyagwa. 8Basi mambo yote ya Yehoahazi yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, na ushujaa wake, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli? 9Yehoahazi akalala na babaze; wakamzika katika Samaria. Na Yehoashi#13:9 Au, Yoashi. mwanawe akatawala mahali pake.
Yehoashi atawala Israeli
10Katika mwaka wa thelathini na saba wa Yoashi mfalme wa Yuda, Yehoashi mwana wa Yehoahazi alianza kutawala juu ya Israeli katika Samaria, akatawala miaka kumi na sita. 11Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA; hakuyaacha makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli; lakini akaendelea katika hayo. 12#2 Fal 14:9,15; 2 Nya 25:17 Basi mambo yote ya Yehoashi yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, na ushujaa wake aliopigania na Amazia mfalme wa Yuda, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli? 13Yehoashi akalala na babaze; na Yeroboamu akakaa katika kiti chake cha enzi; naye Yehoashi akazikwa huko Samaria, pamoja na wafalme wa Israeli.
Kifo cha Elisha
14 # 2 Fal 2:12; Ayu 22:30 Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akateremka amtazame, akamlilia mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi wake! 15Elisha akamwambia, Twaa uta na mishale; naye akatwaa uta na mishale. 16#Mwa 49:24; 2 Fal 4:34 Akamwambia mfalme wa Israeli, Weka mkono wako katika uta; naye akaweka mkono wake juu yake. Elisha akaweka mikono yake juu ya mikono ya mfalme. 17#1 Fal 20:26 Akasema, Lifungue dirisha linaloelekea mashariki; akalifungua. Basi Elisha akasema, Piga; akapiga. Akasema, Mshale wa BWANA wa kushinda, naam, mshale wa kushinda Shamu, kwa maana utawapiga Washami katika Afeki hata utakapowaangamiza. 18#Kut 17:11 Akasema, Itwae mishale; akaitwaa. Akamwambia mfalme wa Israeli, Piga chini; akaipiga nchi mara tatu, akaacha. 19Yule mtu wa Mungu akamkasirikia, akasema, Ingalikupasa kupiga mara tano au mara sita; ndipo ungaliipiga Shamu hata kuiangamiza; bali sasa utaipiga Shamu mara tatu tu.
20 # 2 Fal 5:2; 6:33 Elisha akafa, nao wakamzika. Basi vikosi vya Wamoabi wakaingia katika nchi mwanzo wa mwaka. 21#2 Fal 4:35; Mt 27:52; Yn 5:25-29 Ikawa, walipokuwa wakimzika mtu, angalia, waliona kikosi; wakamtupa yule mtu kaburini mwa Elisha; mara yule maiti alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka, akasimama kwa miguu.
Israeli wateka miji ya Aramu
22 # 2 Fal 8:12 Na Hazaeli mfalme wa Shamu akawaonea Israeli siku zote za Yehoahazi. 23#Kut 33:19; Amu 10:16; Neh 9:31; 2 Fal 14:27; Isa 30:18,19; Yer 12:15; Omb 3:32; Eze 20:9; Kut 2:24,25; 32:13; Mik 7:20; Lk 1:54,55,72,73 Lakini BWANA akawahurumia, akawasikitikia, na kuwaangalia, kwa ajili ya agano lake na Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, wala hakutaka kuwaangamiza, wala hakuwatupa usoni pake bado. 24Akafa Hazaeli mfalme wa Shamu, na Ben-hadadi mwanawe akatawala mahali pake. 25#2 Fal 18:19 Naye Yehoashi, mwana wa Yehoahazi, akaitwaa tena mkononi mwa Ben-hadadi mwana wa Hazaeli miji ile aliyoitwaa yeye mkononi mwa Yehoahazi baba yake vitani. Mara tatu Yehoashi akamshinda, akairudisha miji ya Israeli.

Iliyochaguliwa sasa

2 Wafalme 13: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia