2 Mambo ya Nyakati 4
4
Mapambo ya hekalu
1 #
Kut 27:1; 1 Fal 9:25; 2 Fal 16:14; Eze 43:13 Tena akafanya madhabahu ya shaba, dhiraa ishirini urefu wake, na dhiraa ishirini upana wake, na dhiraa kumi kwenda juu kwake. 2#Kut 30:18; 1 Fal 7:23 Tena akaifanya bahari ya kusubu,#4:2 ‘Tangi la maji’ dhiraa kumi toka ukingo hadi ukingo, ya mviringo, na kwenda juu kwake ilikuwa dhiraa tano; na uzi wa dhiraa thelathini kuizunguka kabisa. 3#1 Fal 7:24 Na chini yake palikuwa na mifano ya fahali,#4:3 Au, maboga (1 Fal 7:24). walioizunguka pande zote, kwa dhiraa kumi, wakiizunguka pande zote ile bahari. Fahali#4:3 Tazama 4:2. walikuwa safu mbili, wakayeyushwa hapo ilipoyeyushwa hiyo bahari.#4:3 Tazama 4:2. 4Ikakaa juu ya ng'ombe kumi na wawili, watatu wakitazama kaskazini, na watatu wakitazama magharibi, na watatu wakitazama kusini, na watatu wakitazama mashariki; na bahari iliwekwa juu yao, na pande zao za nyuma zote zilikuwa ndani. 5#1 Fal 7:26 Na unene wake ulikuwa nyanda nne, na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi#4:5 Tazama 2:10. elfu tatu, kukaa ndani yake. 6#1 Fal 7:38; Ebr 9:9 Akafanya na birika kumi, akaziweka tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto, za kuoshea; ndizo walizooshea mambo ya kafara; lakini hiyo bahari ilikuwa ya makuhani ya kuogea. 7#1 Fal 7:49; Kut 25:31 Alivitengeneza vinara vya taa kumi vya dhahabu, kama vilivyoagiziwa; akavitia hekaluni, vitano upande wa kulia, na vitano upande wa kushoto. 8#1 Fal 7:48 Akatengeneza na meza kumi, akazitia hekaluni, tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto. Kisha akafanya mabakuli mia moja ya dhahabu. 9#1 Fal 6:36 Tena akatengeneza ua wa makuhani, na ua mkubwa, nayo milango yake, akaifunikiza kwa shaba milango yake. 10#1 Fal 7:39 Nayo bahari akaiweka upande wa kulia kwa mashariki, kuelekea kusini. 11#1 Fal 7:40 Na Huramu akatengeneza vyungu, sepetu, na mabeseni.
Basi Huramu akamaliza kufanya hiyo kazi, aliyomfanyia mfalme Sulemani ya nyumba ya Mungu; 12#1 Fal 7:41 zile nguzo mbili, na mabakuli, na mataji mawili yaliyokuwa juu ya nguzo; nazo nyavu mbili za kuyafunika mabakuli mawili ya mataji yaliyokuwa juu ya nguzo; 13#Kut 28:33,34; 1 Fal 7:20; Wim 4:13; Yer 52:23 na makomamanga mia nne ya nyavu mbili; safu mbili za makomamanga kwa kila wavu, kuyafunika mabakuli mawili ya mataji yalikuwa juu ya nguzo. 14#1 Fal 7:27,43 Akatengeneza vitako, akatengeneza na mabeseni juu ya vitako; 15mafahali kumi na wawili chini yake. 16#1 Fal 7:14,45 Vyungu, pia sepetu, nyuma na vyombo vingine vyote, Huram-abi#4:16 Au, Huramu babaye. akamtengenezea mfalme Sulemani kwa ajili ya nyumba ya BWANA, vilikuwa vya shaba iliyong'arishwa. 17#1 Fal 7:46 Katika uwanda wa Yordani ndipo mfalme alipovisubu, katika udongo mzito kati ya Sukothi na Sereda. 18#1 Fal 7:47 Ndivyo Sulemani alitengeneza vyombo hivi vikiwa vingi sana, uzani wa shaba lliyotumika haukujulikana. 19#1 Fal 7:48-50; 2 Fal 24:13; Yer 28:3; Dan 5:2,3; Kut 25:30; 1 Nya 28:16 Basi Sulemani akavifanya vyombo vyote vilivyokuwamo nyumbani mwa Mungu, madhabahu ya dhahabu pia, nazo meza, ambazo juu yake iliwekwa mikate ya wonyesho; 20#Kut 27:20,21 na vinara na taa zake, ziwake kama ilivyoagizwa mbele ya chumba cha ndani, vya dhahabu iliyosafika; 21#Kut 25:31; 37:20; 1 Fal 6:18-35 na maua, na taa, na makoleo, ya dhahabu, ndiyo dhahabu bora; 22#1 Fal 6:31 na mikasi, na mabakuli, na miiko, na vyetezo, vya dhahabu iliyosafika; na kwa habari za mahali pa kuingia nyumbani, milango yake ya ndani ya patakatifu pa patakatifu, na milango ya nyumba, yaani ya hekalu, ilikuwa ya dhahabu.
Iliyochaguliwa sasa
2 Mambo ya Nyakati 4: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.