Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Mambo ya Nyakati 21

21
Yehoramu atawala
1Yehoshafati akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze katika mji wa Daudi; Yehoramu mwanawe akatawala mahali pake. 2Naye alikuwa na ndugu, wana wa Yehoshafati, Azaria, Yehieli, Zekaria, Azaria, Mikaeli, na Shefatia; hao wote walikuwa wana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda.#21:2 Makala ya Kiebrania ni Israeli. 3Baba yao akawapa zawadi kubwa, za fedha, za dhahabu, na za tunu, pamoja na miji yenye maboma katika Yuda; lakini ufalme akampa Yehoramu, kwa sababu alikuwa mzaliwa wa kwanza. 4#Mwa 4:8; Amu 9:5; 1 Yoh 3:12 Basi Yehoramu alipoinuliwa juu ya ufalme wa babaye, na kujiimarisha, akawaua nduguze wote kwa upanga, na baadhi ya wakuu wa Israeli pia. 5Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipoanza kutawala, akatawala miaka minane huko Yerusalemu. 6#2 Fal 8:18; 2 Nya 18:1; 22:2; Neh 13:26 Akaiendea njia ya wafalme wa Israeli, kama walivyofanya nyumba ya Ahabu; kwa kuwa alikuwa amemwoa binti Ahabu; akafanya maovu machoni pa BWANA. 7#2 Sam 7:12,13; 1 Fal 11:36; 2 Fal 8:19; Zab 132:11 Walakini BWANA hakupenda kuiharibu nyumba ya Daudi, kwa sababu ya agano alilolifanya na Daudi, na kama alivyomwahidi kuwa atampa taa, yeye na wazao wake siku zote.
Uasi wa Edomu
8 # Mwa 27:40; 2 Fal 8:20; 9:22; Zab 106:39; Ufu 17:1-5 Wakati wa enzi zake Edomu wakaasi utawala wa Yuda, wakajifanyia mfalme. 9Ndipo Yehoramu akavuka na makamanda wake, na magari yake yote pamoja naye; akaondoka usiku, akawapiga Waedomi waliomzunguka yeye na hao makamanda wa magari. 10#Mwa 27:40 Hivyo Edomu wakaasi utawala wa Yuda hata leo; wakati huo uo nao Libna wakaasi utawala wake: kwa sababu alikuwa amemwacha BWANA, Mungu wa baba zake.
Barua ya Eliya
11 # Law 17:7; 20:5 Tena ndiye aliyetengeneza mahali pa juu katika milima ya Yuda, na kuongoza wakazi wa Yerusalemu kukosa uaminifu na kufanya Yuda ipotoke. 12Barua kutoka nabii Eliya ilimjia, ikisema, BWANA, Mungu wa Daudi baba yako, asema hivi, Kwa kuwa hukuziendea njia za Yehoshafati baba yako, wala njia za Asa mfalme wa Yuda; 13#Kut 34:15; 2 Fal 9:22 lakini umeiendea njia ya wafalme wa Israeli, ukawaongoza Yuda na wakazi wa Yerusalemu kwenye kukosa uaminifu, kama walivyofanya nyumba ya Ahabu; tena umewaua ndugu zako wa nyumba ya baba yako, waliokuwa wema kuliko wewe; 14tazama, BWANA atawapiga pigo kubwa watu wako, na watoto wako, na wake zako, na mali yako yote; 15nawe utakuwa na ugonjwa mkuu kwa maradhi ya matumbo, yatakapotokea matumbo yako kwa sababu ya ugonjwa huo siku kwa siku. 16#2 Sam 24:1; 1 Fal 11:14,23; 2 Nya 22:1 BWANA akawaamsha roho Wafilisti, na Waarabu walioelekeana na Wakushi juu ya Yehoramu, 17#2 Nya 24:7 nao wakakwea juu ya Yuda, wakaipenya, wakaichukua mali yote iliyoonekama nyumbani mwa mfalme, na wanawe pia, na wakeze; asibakizwe mtoto hata mmoja, ila Ahazia,#21:17 Au, Yehoahazi. aliyekuwa mdogo miongoni mwa wanawe.
Ugonjwa na kifo cha Yehoramu
18Na baada ya hayo yote BWANA akampiga matumbo kwa ugonjwa usioponyeka. 19Ikawa baada ya siku, kufika mwisho wa mwaka wa pili, matumbo yake yakatokea kwa sababu ya ugonjwa wake, akafa akiwa kwenye maumivu makali. Wala watu wake hawakuwasha moto kuombolezea kifo chake kama walivyowafanyia baba zake. 20Alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipoanza kutawala, akatawala huko Yerusalemu miaka minane; akafariki bila kutamaniwa; wakamzika mjini mwa Daudi, ila si katika makaburi ya wafalme.

Iliyochaguliwa sasa

2 Mambo ya Nyakati 21: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia