Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Mambo ya Nyakati 11

11
Yuda na Benyamini wajiimarisha
1 # 1 Fal 12:21 Hata Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba ya Yuda na Benyamini, watu wateule elfu mia moja na themanini waliokuwa hodari, watu wa vita, ili wapigane juu ya Israeli, ili wamrudishie Rehoboamu huo ufalme. 2#Kum 33:1; 1 Sam 2:27; 1 Fal 12:22-24; 2 Nya 8:14; 12:15; 1 Tim 6:11 Lakini neno la BWANA likamjia Shemaya mtu wa Mungu, kusema, 3Mwambie Rehoboamu mwana wa Sulemani, mfalme wa Yuda, uwaambie na Israeli wote waliomo Yuda na Benyamini, ukisema, 4BWANA asema hivi, Hamtapanda wala kupigana na ndugu zenu; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi wakayatii maneno ya BWANA wakarudi wasiende kupigana na Yeroboamu.
5Naye Rehoboamu akakaa Yerusalemu, akajenga miji yenye ngome katika Yuda. 6#Mwa 35:19; 1 Sam 17:12; Mt 2:1; Amu 15:8; 1 Nya 4:31; 2 Sam 14:2; 2 Nya 20:20; Neh 3:5; Yer 6:1; Amo 1:1 Akajenga Bethlehemu, Etamu, Tekoa, 7Beth-suri, Soko, Adulamu, 8Gathi, Maresha, Zifu, 9Adoraimu, Lakishi, Azeka, 10Sora, Aiyaloni, na Hebroni, iliyoko katika Yuda na Benyamini, miji yenye maboma. 11Akazifanya imara hizo ngome, akaweka majemadari humo, na akiba ya vyakula, na mafuta, na mvinyo. 12Na ndani ya miji yote mmoja mmoja aliweka ngao na mikuki, akaifanya kuwa na nguvu nyingi mno. Yuda na Benyamini ikawa milki yake.
Makuhani na Walawi aamuunga Rehoboamu mkono
13Makuhani na Walawi waliokuwa katika Israeli yote wakamwendea, kutoka maeneo yao yote. 14#Hes 35:2; Yos 21:20-42; 1 Fal 12:28-33; 2 Nya 13:9 Walawi wakaacha malisho yao, na milki yao, wakaja Yuda na Yerusalemu; kwa sababu Yeroboamu na wanawe waliwakataza, ili wasimfanyie BWANA ukuhani; 15#1 Fal 12:31; 13:33; 14:9; Hos 13:2; Law 17:7; Kum 32:15-17; 1 Kor 10:20; Ufu 16:14; 1 Fal 12:28 naye akajiwekea makuhani wa mahali pa juu, na wa wale majini, na wa zile ndama alizozitengeneza. 16#2 Nya 15:9; 30:11; Zab 69:32 Na kutoka katika kabila zote za Israeli, wakaandamwa na hao waliojikaza nia kumtafuta BWANA, Mungu wa Israeli, wakaja Yerusalemu, ili wamtolee dhabihu BWANA, Mungu wa baba zao. 17#2 Nya 12:1; Hos 6:4; Mt 13:18 Hivyo wakaufanya imara kwa miaka mitatu ufalme wa Yuda, na kumtia nguvu Rehoboamu mwana wa Sulemani; kwa maana muda wa miaka mitatu wakaiendea njia ya Daudi na Sulemani.
Ndoa za Rehoboamu
18Rehoboamu akaoa mke, Mahalathi binti Yerimothi mwana wa Daudi, na wa Abihaili binti Eliabu, mwana wa Yese; 19#1 Fal 15:2 akamzalia wana, Yeushi, na Shemaria, na Zahamu. 20Kisha baada yake akamwoa Maaka, binti Absalomu; na yeye akamzalia Abiya, na Atai, na Ziza, na Shelomithi. 21Rehoboamu akampenda Maaka binti Absalomu kuliko wakeze wote na masuria yake; (maana alioa wake kumi na wanane, na masuria sitini, akazaa watoto wa kiume ishirini na wanane na mabinti sitini). 22#Kum 21:15-17 Rehoboamu akamteua Abiya, mwana wa Maaka, kuwa mkuu, mtawala kati ya nduguze, kwa kuwa aliazimia kumtawaza awe mfalme. 23#Kum 17:17; 1 Fal 11:3 Akafanya kwa akili, akawatawanya wanawe wote kati ya nchi zote za Yuda na Benyamini, katika kila mji wenye boma; akawapa vyakula tele. Akawatafutia wake wengi.

Iliyochaguliwa sasa

2 Mambo ya Nyakati 11: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia