Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Samweli 8:5-9

1 Samweli 8:5-9 SRUV

wakamwambia, Angalia, wewe umezeeka, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tuteulie mfalme atutawale kama mataifa yale mengine yote. Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba BWANA. BWANA akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao. Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe. Basi sasa, isikilize sauti yao; lakini, uwaonye sana, na kuwaonesha desturi ya mfalme atakayewamiliki.

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha