Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Samweli 31:1-6

1 Samweli 31:1-6 SRUV

Basi Wafilisti wakapigana na Israeli; nao watu wa Israeli wakawakimbia Wafilisti, wakauawa katika mlima wa Gilboa. Wafilisti wakamfuatia sana Sauli na wanawe, Wafilisti wakawaua Yonathani, na Abinadabu, na Malkishua, wana wa Sauli. Tena vita vilikuwa vikali sana juu ya Sauli, na wapiga upinde wakampata; hata akafadhaika sana kwa sababu ya wapiga upinde. Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao; wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanichoma, na kunisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia. Na mchukua silaha zake alipoona ya kuwa Sauli amekufa, yeye naye akauangukia upanga wake, akafa pamoja naye. Hivyo Sauli akafa, na wanawe watatu, na mchukua silaha zake, na watu wake wote pamoja siku iyo hiyo.