Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Samweli 17:32-36

1 Samweli 17:32-36 SRUV

Daudi akamwambia Sauli, Asifadhaike moyo mtu yeyote kwa ajili ya huyu; mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Huwezi kumwendea Mfilisti huyu upigane naye; maana wewe ni kijana tu; na huyu ni mtu wa vita tangu ujana wake. Daudi akamwambia Sauli, Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake, na alipokuwa akija simba, au dubu, akamkamata mwana-kondoo wa lile kundi, mimi hutoka nikamfuata, nikampiga, nikampokonya kinywani mwake; na akinirukia, humshika ndevu zake, nikampiga, nikamwua. Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 1 Samweli 17:32-36