1 Wakorintho 1:12-14
1 Wakorintho 1:12-14 SRUV
Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo. Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulubiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo? Nashukuru, kwa sababu sikumbatiza mtu kwenu, ila Krispo na Gayo