Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mambo ya Nyakati 26

26
Mabawabu wa hekalu
1 # Hes 16:1,2; 26:9-11; 1 Nya 9:17; 15:18; 2 Nya 23:19; Yud 1:11; 1 Nya 6:39 Kwa zamu zao mabawabu; wa Wakora; Meshelemia mwana wa Kore, wa wana wa Ebiasafu. 2Naye Meshelemia alikuwa na wana; Zekaria mzaliwa wa kwanza, Yediaeli wa pili, Zebadia wa tatu, Yathnieli wa nne; 3Elamu wa tano, Yohana wa sita, Elioenai wa saba. 4Naye Obed-edomu alikuwa na wana; Shemaya mzaliwa wa kwanza, Yehozabadi wa pili, Yoa wa tatu, na Sakari wa nne, na Nethaneli wa tano; 5#1 Nya 13:14; Mwa 33:5; Zab 127:3 Amieli wa sita, Isakari wa saba, Peulethai wa nane; kwa jinsi Mungu alivyombariki. 6Naye mwanawe Shemaya akazaliwa wana, walioongoza ukoo wa baba yao; kwa kuwa walikuwa wanaume mashujaa. 7Wana wa Shemaya; Othni, na Refaeli, na Obedi, na Elzabadi, nduguze walikuwa mashujaa, Elihu, na Semakia. 8Hao wote walikuwa wana wa Obed-edomu; wao na wana wao na ndugu zao, watu hodari wawezao huo utumishi; watu wa Obed-edomu sitini na wawili. 9Naye Meshelemia alikuwa na wana na nduguze, watu mashujaa, kumi na wanane. 10#1 Nya 16:38; Mwa 4:7; 49:3; Kum 21:17; 1 Nya 5:1 Hosa naye, wa wana wa Merari, alikuwa na wana; Shimri mkuu wao; (kwani ajapokuwa yeye si mzaliwa wa kwanza, babaye alimweka mkuu); 11Hilkia wa pili, Tebalia wa tatu, Zekaria wa nne; wana wote wa Hosa pamoja na nduguze walikuwa watu kumi na watatu. 12Katika hao zilikuwa zamu za mabawabu, yaani, katika hao wakuu, wenye huduma kama ndugu zao, wa kutumika katika nyumba ya BWANA. 13#Yos 18:10; 1 Nya 25:8; 24:5; Mit 18:18; Yon 1:7; Mdo 1:26; 10:34; Gal 3:28; Kol 3:11 Nao wakapigiwa kura kwa ajili ya kila lango, wadogo na wakubwa kwa pamoja, kwa kufuata koo za baba zao. 14Kura ya lango la mashariki ikamwangukia Meshelemia. Ndipo wakamtupia kura Zekaria mwanawe, mshauri mwenye busara; na kura yake ikamtokea ya kaskazini. 15Ya Obed-edomu ya kusini; na ya wanawe nyumba ya akiba. 16#1 Fal 10:5; 1 Nya 24:31; 25:8; 2 Nya 9:4; Neh 12:24 Ya Shupimu na Hosa upande wa magharibi, langoni pa Shalekethi, hapo penye daraja ya kupandia, ulinzi ulifanywa kwa zamu. 17Upande wa mashariki walikuwapo Walawi sita, kaskazini wanne kila siku, kusini wanne kila siku, na wa nyumba ya akiba wawili wawili. 18Penye Parbari upande wa magharibi, walikuwapo wanne darajani, na wawili huko Parbari. 19Hizo ndizo zamu za mabawabu; wa wana wa Wakora, na wa wana wa Merari.
Watunza hazina, maofisa na waamuzi
20 # Kum 12:6; 1 Fal 7:51; 14:26; 1 Nya 9:26-29; 22:14-16; Mal 3:10; 2 Nya 31:11,12 Na katika Walawi; Ahia mtunzaji wa hazina ya nyumba ya Mungu, pamoja na hazina ya vitu vilivyowekwa wakfu. 21#1 Nya 6:17; 23:8 Wana wa Ladani; wana wa Wagershoni waliokuwa wa Ladani; wakuu wa koo za mababa waliokuwa wa Ladani, Mgershoni; Yehieli. 22Wana wa Yehieli; Zethamu, na Yoeli nduguye, walikuwa watunzaji wa hazina ya nyumba ya BWANA. 23#Kut 6:18; Hes 3:19; 1 Nya 23:12 Wa Waamrami wa Waishari, wa Wahebroni, wa Wauzieli; 24#1 Nya 23:16; 24:20 na Shebueli, mwana wa Gershomu, mwana wa Musa, alikuwa mtunzaji wa hazina zote. 25#1 Nya 23:18; 24:22 Na nduguze; wa Eliezeri, Rehabia mwanawe, na Ishia mwanawe, na Yoramu mwanawe, na Zikri mwanawe, na Shelomothi mwanawe. 26Huyo Shelomothi na ndugu zake walikuwa wasimamizi wa hazina zote za vitu vilivyowekwa wakfu, alivyoviweka wakfu mfalme Daudi, na hao wakuu wa koo za mababa, na maofisa wa maelfu na wa mamia, na makamanda wa jeshi. 27#Hes 31:50; Yos 6:19,24; 1 Nya 22:14-16; 2 Nya 15:11,18; 2 Fal 12:14; 22:4,5; Neh 10:32 Katika nyara zilizopatikana vitani, waliweka wakfu sehemu, ili kuitengeneza nyumba ya BWANA. 28#1 Sam 9:9 Na vyote alivyoviweka wakfu Samweli mwonaji, na Sauli mwana wa Kishi, na Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Seruya; na mtu yeyote aliyekiweka wakfu kitu chochote, kilikuwa chini ya mkono wa Shelomothi na nduguze.
29 # Kum 1:16; 16:18; 1 Nya 23:4; 2 Nya 19:8-11 Katika Waishari, Kenania na wanawe walikuwa kwa ajili ya kazi ya nje juu ya Israeli, kuwa maofisa na waamuzi. 30Katika Wahebroni, Hashabia na nduguze, mashujaa, elfu moja na mia saba, walikuwa na usimamizi juu ya Israeli ng'ambo ya Yordani upande wa magharibi; kwa ajili ya kazi zote za BWANA, na kwa utumishi wa mfalme. 31#1 Nya 23:19; 2 Sam 5:4; 1 Fal 2:11; 1 Nya 29:27; Hes 32:1,3,35; Yos 21:39; Isa 16:9; Yer 48:32 Katika Wahebroni Yeria alikuwa mkuu, yaani, wa hao Wahebroni kwa kufuata vizazi vyao kwa koo za mababa. Katika mwaka arubaini wa kutawala kwake Daudi wakatafutwa, wakaonekana huko Yazeri ya Gileadi miongoni mwao wanaume mashujaa. 32#2 Nya 19:11 Na nduguze, mashujaa, walikuwa elfu mbili na mia saba, wakuu wa koo za mababa, ambao mfalme Daudi aliwaweka wawe wasimamizi juu ya Wareubeni, na Wagadi, na nusu kabila la Wamanase, kwa ajili ya kila neno lililomhusu Mungu, na kwa mambo ya mfalme.

Iliyochaguliwa sasa

1 Mambo ya Nyakati 26: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia