1 Mambo ya Nyakati 16
16
Sanduku la Bwana Lawekwa katika Hema
1 #
2 Sam 6:17-19
Wakaliingiza sanduku la Mungu, na kuliweka katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake; wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu. 2Na Daudi alipokwisha kuitoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la BWANA. 3Kisha akawagawia kila mtu wa Israeli, wanaume kwa wanawake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu.
4Akawaagiza baadhi ya Walawi kwamba watumike mbele ya sanduku la BWANA, wamfanyie ukumbusho, na shukrani, na sifa, BWANA, Mungu wa Israeli; 5Asafu mkuu wao, na wa pili wake Zekaria, na Yeieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Metithia, na Eliabu, na Benaya, na Obed-edomu, na Yeieli, wenye vinanda na vinubi; naye Asafu mwenye kupiga matoazi; 6nao makuhani Benaya na Yahazieli wenye baragumu daima, mbele ya sanduku la Agano la Mungu.
Daudi aimba wimbo wa shukrani
7 #
2 Sam 23:1
Ndipo siku hiyo Daudi alipoagiza kwanza kumshukuru BWANA, kwa mkono wa Asafu na nduguze.
8 #
Zab 105:1; 145:1 Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake;
Wajulisheni watu matendo yake.
9 #
Zab 95:1,2; 100:1 Mwimbieni, mwimbieni nyimbo za kumsifu;
Yatangazeni matendo yake yote ya ajabu.
10 #
Zab 34:3; Isa 45:25 Jisifuni kwa jina lake takatifu;
Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA.
11 #
Amo 5:6,14 Mtafuteni BWANA na nguvu zake;
Utafuteni uso wake siku zote.
12 #
Zab 103:2; 111:2 Yakumbukeni matendo yake yote ya ajabu aliyoyafanya;
Miujiza yake na hukumu za kinywa chake;
13Enyi wazao wa Israeli, mtumishi wake,
Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
14Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu;
Duniani kote kuna hukumu zake.
15Likumbukeni agano lake milele,
Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.
16 #
Mwa 15:18; 17:2; 26:3; Neh 9:8; Ebr 6:13-18 Agano alilofanya na Abrahamu,
Na kiapo chake kwa Isaka;
17Aliyomthibitishia Yakobo kuwa amri,
Na kwa Israeli kuwa agano la milele.
18Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani,
Iwe urithi wenu mliopimiwa;
19 #
Mwa 34:30; Ebr 11:13 Mlipokuwa watu wawezao kuhesabiwa;
Naam, watu wachache na wageni ndani yake.
20Mkitangatanga toka taifa hadi taifa,
Toka ufalme mmoja hadi kwa watu wengine.
21 #
Mwa 12:17; 20:3; Kut 7:15-18 Hakumwacha mtu awaonee;
Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao;
22 #
Zab 105:15; 1 Yoh 2:27 Akisema, Msiwaguse masihi#16:22 Au mtiwa mafuta (tazama 1 Sam 2:10). wangu,
Wala msiwadhuru nabii zangu.
23 #
Zab 47:1; 96:1 Mwimbieni BWANA, nchi yote;
Tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.
24 #
Isa 12:4
Watangazieni mataifa habari za utukufu wake,
Na watu wote habari za maajabu yake.
25 #
Zab 24:8; 89:6-8; Isa 40:25,26 Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana;
Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.
26 #
Law 19:4; Zab 115:4-8; Isa 45:20; Yer 10:3; 1 Kor 8:4 Maana miungu yote ya watu si kitu;
Lakini BWANA ndiye aliyezifanya mbingu.
27 #
Zab 8:1
Heshima na adhama ziko mbele zake;
Nguvu na furaha zipo mahali pake.
28Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu,
Mpeni BWANA utukufu na nguvu.
29Mpeni BWANA utukufu wa jina lake;
Leteni sadaka, na mje mbele zake;
Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu;
30Tetemekeni mbele zake, nchi yote.
Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;
31 #
Isa 35:10; Lk 2:13; Ufu 14:2 Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie;
Na waseme katika mataifa, BWANA ametamalaki;
32 #
Zab 96:10
Bahari na ivume na vyote viijazavyo;
Mashamba na yashangilie na vyote vilivyomo;
33Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha,
Mbele za BWANA,
Kwa maana anakuja kuihukumu nchi.
34 #
Zab 106:1; 107:1; 118:1 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
35 #
Zab 106:47,48 Nanyi semeni,
Ee Mungu wa wokovu wetu, utuokoe,
Utukusanye kwa kututoa katika mataifa,
Tulishukuru jina lako takatifu,
Tuzifanyie shangwe sifa zako.
36 #
1 Fal 8:15; Zab 72:18,19; Kum 27:15; Neh 8:6 Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli, tangu milele hata milele. Na watu wote wakasema, Amina; wakamhimidi BWANA.
Ibada zarejeshwa tena
37Basi akawaacha huko, mbele ya sanduku la Agano la BWANA, Asafu na nduguze, ili watumike mbele ya sanduku daima, kila siku kama ilivyokuwa kazi yake. 38Naye Obed-edomu, pamoja na ndugu zao, sitini na wanane; Obed-edomu na mwana wa Yeduthuni, na Hosa, wawe mabawabu; 39#1 Nya 21:29; 2 Nya 1:3; 1 Fal 3:4 na Sadoki kuhani, na nduguze makuhani, mbele ya maskani ya BWANA katika mahali pa juu palipokuwa huko Gibeoni, 40#Kut 29:38; Hes 28:3 ili kumtolea BWANA sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa daima asubuhi na jioni, naam, kulingana na yote yaliyoandikwa katika Torati ya BWANA, aliyowaamuru Israeli; 41#2 Nya 5:13; 7:3; Ezr 3:11; Neh 9:17; Zab 25:10; 33:5; 100:5; Yer 33:11; Yoe 2:13; Lk 6:36; Yak 5:11 na pamoja nao Hemani na Yeduthuni, na wale wengine waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru BWANA, kwa kuwa fadhili zake ni za milele; 42na pamoja nao Hemani na Yeduthuni wenye baragumu na matoazi, kwa hao watakaovumisha sauti, na vinanda kwa ajili ya hizo nyimbo za Mungu; na hao wana wa Yeduthuni wawepo mlangoni. 43#2 Sam 6:19,20; Mwa 18:19; Yos 24:15 Kisha watu wote wakaenda zao kila mtu nyumbani kwake; naye Daudi akarudi ili awabariki watu wa nyumbani mwake.
Iliyochaguliwa sasa
1 Mambo ya Nyakati 16: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.