Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mambo ya Nyakati 13

13
Sanduku la Agano laletwa kutoka Kiriath-yearimu
1 # 2 Sam 5:1; 6:1; 1 Fal 8:1; 1 Nya 12:14; Zab 132:1; Mit 15:22 Kisha Daudi akafanya shauri na makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, naam, na kila kiongozi. 2#1 Nya 10:7; Isa 37:4 Daudi akawaambia jamii yote ya Israeli, Likiwa jema kwenu, tena likiwa limetoka kwa BWANA, Mungu wetu, na tutume watu huku na huku mahali pote kwa ndugu zetu waliosalia katika nchi yote ya Israeli, ambao pamoja nao makuhani na Walawi wamo ndani ya miji yao yenye viunga, ili wakusanyike kwetu; 3#1 Sam 7:1; 14:18; 23:2,4 nasi tujirudishie tena sanduku la Mungu wetu; maana hatukulitilia maanani katika siku za Sauli. 4Nao jamii nzima wakasema ya kwamba watafanya hivyo; kwa kuwa neno hilo lilikuwa jema machoni pa watu wote. 5#2 Sam 6:1; Yos 13:3; 1 Sam 6:21; 7:1 Basi Daudi akawakusanya Israeli wote, toka Shihori, kijito cha Misri, hadi pa kuingilia Hamathi, ili walilete sanduku la Mungu kutoka Kiriath-yearimu. 6#Yos 15:9,60; Kut 25:22; 1 Sam 4:4 Basi Daudi akapanda, yeye na Israeli wote, mpaka Baala, ndio Kiriath-yearimu, ulio wa Yuda, ili kulileta toka huko sanduku la Mungu, BWANA akaaye juu ya makerubi, lililoitwa kwa Jina lake. 7#Hes 4:15 Wakalipandisha sanduku la Mungu juu ya gari jipya kutoka nyumba ya Abinadabu; na Uza na Ahio wakaliendesha lile gari. 8#2 Sam 6:5 Wakacheza Daudi na Israeli wote, mbele za Mungu, kwa nguvu zao zote; na kwa nyimbo na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa matoazi, na kwa tarumbeta. 9#2 Sam 6:6 Hata walipofika penye uga wa Nakoni, Uza akaunyosha mkono wake alishike sanduku; kwa maana wale ng'ombe walijikwaa. 10#Hes 4:15; 1 Nya 15:13,15; Law 10:2 Ndipo hasira ya BWANA ikawaka juu ya Uza, naye akampiga, kwa sababu alilinyoshea sanduku mkono wake, hadi akafa pale pale mbele za Mungu. 11Naye Daudi akaona uchungu, kwa kuwa BWANA amemfurikia Uza; akapaita mahali pale Peres-uza#13:11 Tazama 2 Sam 6:8 hata leo. 12Naye Daudi akamwogopa Mungu siku ile, akasema, Nitajileteaje sanduku la Mungu kwangu? 13Basi Daudi hakujichukulia sanduku mjini mwa Daudi, ila akalihamisha kando na kulitia nyumbani kwa Obed-edomu, Mgiti. 14#2 Sam 6:11; Mwa 30:27; 39:5; 1 Nya 26:5; Zab 37:22; Mit 3:9; 10:22; Mal 3:10 Sanduku la Mungu likakaa na jamaa ya Obed-edomu, nyumbani mwake, muda wa miezi mitatu; naye BWANA akaibariki nyumba ya Obed-edomu, na yote aliyokuwa nayo.

Iliyochaguliwa sasa

1 Mambo ya Nyakati 13: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia