Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 25

25
Sala ya uongozi na ukombozi
Zaburi ya Daudi.
1 # 1 Sam 1:15; Zab 86:4; Omb 3:41 Ee BWANA, nakuinulia nafsi yangu,
2 # Zab 7:1; 18:2; Rum 10:11 Ee Mungu wangu,
Nimekutumainia Wewe, nisiaibike,
Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda.
3Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja;
Wataaibika watendao uhaini bila sababu.
4 # Kut 33:13; Zab 143:8; Mit 8:20 Ee BWANA, unijulishe njia zako,
Unifundishe mapito yako,
5Uniongoze katika kweli yako,
Na kunifundisha.
Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu,
Nakungoja Wewe mchana kutwa.
6Ee BWANA, kumbuka rehema zako na fadhili zako,
Maana zimekuwako tokea zamani.
7 # Zab 51:1 Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu,
Wala maasi yangu.
Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako,
Ee BWANA kwa ajili ya wema wako.
8BWANA yu mwema, mwenye adili,
Kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi njia.
9Wenye upole atawaongoza katika haki,
Wenye upole atawafundisha njia yake.
10Njia zote za BWANA ni fadhili na kweli,
Kwao walishikao agano lake na shuhuda zake.
11 # Zab 31:3; 79:9; Rum 5:20 Ee BWANA, kwa ajili ya jina lako,
Unisamehe uovu wangu, maana ni mwingi.
12 # Zab 37:23 Ni nani amchaye BWANA?
Atamfundisha katika njia anayoichagua.
13 # Zab 37:11,22,29 Watafanikiwa maishani mwao;
Na wazawa wao wataimiliki nchi.
14 # Mit 3:32; Yn 7:17; 2 Kor 4:2-6 Siri ya BWANA iko kwao wamchao,
Naye atawajulisha agano lake.
15 # Zab 141:8 Macho yangu humwelekea BWANA daima,
Naye atanitoa miguu yangu katika wavu.
16 # Zab 69:16 Uniangalie na kunifadhili,
Maana mimi ni mkiwa na mteswa.
17Uniondolee shida za moyo wangu,
Na kunitoa katika dhiki zangu.
18 # 2 Sam 16:12 Utazame mateso yangu na taabu yangu;
Unisamehe dhambi zangu zote.
19Uwatazame adui zangu, maana ni wengi,
Na kwa namna wanavyonichukia kwa ukatili mwingi.
20Unilinde nafsi yangu na kuniokoa,
Usiniache niaibike, maana nakukimbilia Wewe.
21Ukamilifu na unyofu zinihifadhi,
Maana nakungoja Wewe.
22 # Zab 130:8 Ee Mungu, umkomboe Israeli,
Katika taabu zake zote.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 25: SRUVDC

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia