Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 21

21
Shukrani kwa ushindi
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1Ee BWANA, mfalme atazifurahia nguvu zako,
Na wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana.
2 # Yn 11:42 Umempa haja ya moyo wake,
Wala hukumzuilia matakwa ya midomo yake.
3Maana umemsogezea baraka za heri,
Umemvika taji la dhahabu safi kichwani pake.
4 # 2 Sam 7:19 Alikuomba uhai, ukampa,
Muda mrefu wa siku nyingi, milele na milele.
5Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako,
Heshima na adhama waweka juu yake.
6Maana umemfanya kuwa baraka za milele,
Wamfurahisha kwa furaha ya uso wako.
7 # Zab 91:2 Kwa kuwa mfalme humtumainia BWANA,
Na kwa fadhili zake Aliye Juu hatatikisika.
8Mkono wako utawapata adui zako wote,
Mkono wako wa kulia utawapata wanaokuchukia.
9 # Kum 32:22 Utawafanya kuwa kama tanuri ya moto,
Wakati wa ghadhabu yako.
BWANA atawameza kwa ghadhabu yake,
Na moto utawateketeza.
10Matunda yao utayaharibu na kuyaondoa katika nchi,
Na wazao wao katika wanadamu.
11Wakipanga kukutenda mabaya,
Kwa miango ya hila, hawatafanikiwa.
12Kwa maana utawatimua utawafanya wakimbie,
Kwa upote wa uta wako utazilenga nyuso zao.
13 # Ufu 15:3,4 Ee BWANA, utukuzwe kwa nguvu zako,
Nasi tutaimba na kuuhimidi uwezo wako.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 21: SRUVDC

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia