Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wim 6

6
Uzuri wa Bibi Arusi usio na Kifani
1 # Wim 1:8 Mpendwa wako amekwenda wapi,
Wewe uliye mzuri katika wanawake?
Mpendwa wako amegeukia upande upi,
Ili tumtafute pamoja nawe?
2 # Isa 40:11; Sef 3:17; Ufu 7:17; Isa 56:8; Yn 10:16 Mpendwa wangu ameshukia bustani yake,
Kwenye matuta ya rihani;
Ili kulisha penye bustani,
Ili kuchuma nyinyoro.
3 # Wim 2:16; Ufu 21:2 Mimi ni wake mpendwa wangu, naye ni wangu,
Hulisha kundi lake penye nyinyoro.
4 # 2 Kor 10:4 Mpenzi wangu, u mzuri kama Tirza,
Mwenye kupendeza kama Yerusalemu,
Wa kutisha kama wenye bendera.
5 # Wim 4:1 Uyageuzie macho yako mbali nami,
Kwa maana yamenitisha sana.
Nywele zako ni kama kundi la mbuzi,
Wakijilaza mbavuni pa Gileadi.
6Meno yako kama kundi la kondoo,
Wakipanda kutoka kuoshwa;
Ambao kila mmoja amezaa mapacha,
Wala hakuna aliyefiwa kati yao.
7Mashavu yako ni kama kipande cha komamanga,
Nyuma ya barakoa yako.
8Wako malkia sitini, na masuria themanini,
Na wanawali wasiohesabika;
9Hua wangu, mkamilifu wangu, ni mmoja tu,
Mtoto wa pekee wa mamaye.
Ndiye kipenzi chake aliyemzaa,
Binti wakamwona wakamwita heri;
Malkia na masuria nao wakamwona,
Wakamsifu, wakisema,
10Ni nani huyu atazamaye kama alfajiri,
Mzuri kama mwezi, safi kama jua,
Wa kutisha kama wenye bendera?
11 # Wim 7:12 Nalishukia bustani ya milozi,
Ili kuyatazama machipuko ya bondeni;
Nione kama mzabibu umechanua,
Kama mikomamanga imetoa maua.
12Kabla sijajua, roho yangu ilinileta
Katikati ya magari ya wakuu wangu.
13Rudi, rudi, Mshulami,
Rudi, rudi, ili sisi tukutazame.
Kwani mnataka kumtazama Mshulami,
Kama kutazama ngoma ya Mahanaimu?

Iliyochaguliwa sasa

Wim 6: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha