Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wim 4

4
Uzuri wa Bibi Arusi Watukuzwa
1 # Wim 1:15; 6:5 Tazama, u mzuri, mpenzi wangu,
U mzuri, macho yako ni kama ya hua,
Nyuma ya barakoa yako.
Nywele zako ni kama kundi la mbuzi,
Wakijilaza mbavuni pa mlima Gileadi.
2 # Wim 6:6 Meno yako ni kama kundi waliokatwa manyoya,
Wakipanda kutoka kuoshwa,
Ambao kila mmoja amezaa mapacha,
Wala hakuna aliyefiwa kati yao.
3Midomo yako ni kama uzi mwekundu,
Na kinywa chako ni kizuri;
Mashavu yako ni kama kipande cha komamanga,
Nyuma ya barakoa yako.
4 # 2 Sam 22:51; Wim 1:10; Neh 3:19 Shingo yako ni kama mnara wa Daudi,
Uliojengwa pa kuwekea silaha;
Ngao elfu zimetungikwa juu yake,
Zote ni ngao za mashujaa.
5 # Mit 5:19; Wim 1:13; Isa 66:10-12; 1 Pet 2:2 Maziwa yako mawili ni kama wana-paa wawili,
Nyuma ya barakoa yako.
Ambao ni mapacha ya paa;
Wakilisha penye nyinyoro.
6Hata jua lipunge, na vivuli vikimbie,
Nitakwenda kwenye mlima wa manemane,
Na kwenye kilima cha ubani.
7 # Efe 5:27 Mpenzi wangu, u mzuri pia pia,
Wala ndani yako hamna ila.
8 # Kum 3:9 Bibi arusi, njoo pamoja nami toka Lebanoni,
Pamoja nami toka Lebanoni.
Shuka kutoka kilele cha Amana,
Kutoka vilele vya Seniri na Hermoni;
Kutoka mapangoni mwa simba,
Kutoka milimani mwa chui.
9 # Isa 54:5; Yn 3:29; 2 Kor 11:2; Ufu 19:7,8 Umenishangaza moyo, umbu langu,
Bibi arusi, umenishangaza moyo,
Kwa mtupo mmoja wa macho yako,
Kwa mkufu mmoja wa shingo yako.
10Jinsi zilivyo nzuri pambaja zako, umbu langu,
Bibi arusi, ni nzuri kupita divai;
Na harufu ya marhamu yako
Yapita manukato ya kila namna.
11 # Mit 24:13,14; Mwa 27:27; Hos 14:6,7 Bibi arusi, midomo yako yadondoza asali,
Asali na maziwa vi chini ya ulimi wako;
Na harufu ya mavazi yako
Ni kama harufu ya Lebanoni.
12 # Isa 58:11; Hos 3:3 Bustani iliyofungwa ni umbu langu, bibi arusi,
Kijito kilichofungwa, chemchemi iliyotiwa muhuri.
13Machipuko yako ni bustani ya komamanga,
Yenye matunda mazuri, hina na nardo,
14Nardo na zafarani, mchai na mdalasini,
Na miti yote iletayo ubani,
Manemane na udi, na kolezi kuu zote.
15 # Yn 4:10 Wewe ndiwe chemchemi ya bustani yangu,
Kisima cha maji yaliyo hai,
Vijito vya Lebanoni viendavyo kasi.
16 # Gal 5:22; Wim 5:1 Amka, kaskazi; nawe uje, kusi;
Vumeni juu ya bustani yangu,
Manukato ya bustani yatokee.
Mpendwa wangu na aingie bustanini mwake,
Akayale matunda yake mazuri.

Iliyochaguliwa sasa

Wim 4: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha