Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 8:1-9

Zab 8:1-9 SUV

Wewe, MUNGU, Bwana wetu Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni; Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu; Kwa sababu yao wanaoshindana nawe; Uwakomeshe adui na mijilipiza kisasi. Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha; Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake. Kondoo, na ng’ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni; Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini. Wewe, MUNGU, Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!

Soma Zab 8

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 8:1-9