Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 78:1-7

Zab 78:1-7 SUV

Enyi watu wangu, sikilizeni sheria yangu, Tegeni masikio kwa maneno ya kinywa changu. Na nifunue kinywa changu kwa mithali, Niyatamke mafumbo ya kale. Mambo tuliyoyasikia na kuyafahamu, Ambayo baba zetu walituambia. Hayo hatutawaficha wana wao, Huku tukiwaambia kizazi kingine, Sifa za BWANA, na nguvu zake, Na mambo yake ya ajabu aliyoyafanya. Maana alikaza ushuhuda katika Yakobo, Na sheria aliiweka katika Israeli. Aliyowaamuru baba zetu Wawajulishe wana wao, Ili kizazi kingine wawe na habari, Ndio hao wana watakaozaliwa. Wasimame na kuwaambia wana wao Wamwekee Mungu tumaini lao. Wala wasiyasahau matendo ya Mungu, Bali wazishike amri zake.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 78:1-7