Zab 39
39
Sala ya Kutaka Hekima na Msamaha
Kwa mwimbishaji: kwa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi.
1 #
1 Fal 2:4; Mit 4:26,27; Ebr 2:1; Kol 4:5 Nalisema, Nitazitunza njia zangu
Nisije nikakosa kwa ulimi wangu;
Nitajitia lijamu kinywani,
Maadamu mtu mbaya yupo mbele yangu.
2Nalikuwa sisemi, nalinyamaa kimya,
Sina faraja, maumivu yangu yakazidi.
3 #
Yer 20:9
Moyo wangu ukawa moto ndani yangu,
Na katika kuwaza kwangu moto ukawaka;
Nalisema kwa ulimi wangu,
4BWANA, unijulishe mwisho wangu,
Na kiasi cha siku zangu ni kiasi gani;
Nijue jinsi nilivyo dhaifu.
5 #
Zab 90:4
Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri;
Maisha yangu ni kama si kitu mbele zako.
Kila mwanadamu, ingawa amesitawi, ni ubatili.
6Binadamu huenda tu huko na huko kama kivuli;
Hufanya ghasia tu kwa ajili ya ubatili;
Huweka akiba wala hajui ni nani atakayeichukua.
7Na sasa ninangoja nini, Ee Bwana?
Matumaini yangu ni kwako.
8Uniokoe na maasi yangu yote,
Usinifanye laumu ya mpumbavu.
9Nimenyamaza, sitafumbua kinywa changu,
Maana Wewe ndiwe uliyeyafanya.
10Uniondolee pigo lako;
Kwa uadui wa mkono wako nimeangamia.
11Ukimrudi mtu kwa kumkemea kwa uovu wake,
Watowesha uzuri wake kama nondo.
Kila mwanadamu ni ubatili.
12 #
Law 25:23; 1 Nya 29:15 Ee BWANA, usikie maombi yangu,
Utege sikio lako niliapo,
Usiyanyamalie machozi yangu.
Kwa maana mimi ni mgeni wako,
Msafiri kama baba zangu wote.
13 #
Ayu 10:20,21 Uniachilie nikunjuke uso,
Kabla sijaondoka nisiwepo tena.
Iliyochaguliwa sasa
Zab 39: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.