Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 25:1-9

Zab 25:1-9 SUV

Ee BWANA, nakuinulia nafsi yangu, Ee Mungu wangu, Nimekutumaini Wewe, nisiaibike, Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda. Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja; Wataaibika watendao uhaini bila sababu. Ee BWANA, unijulishe njia zako, Unifundishe mapito yako, Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa. Ee BWANA, kumbuka rehema zako na fadhili zako, Maana zimekuwako tokea zamani. Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu, Wala maasi yangu. Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako, Ee BWANA kwa ajili ya wema wako. BWANA yu mwema, mwenye adili, Kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi njia. Wenye upole atawaongoza katika hukumu, Wenye upole atawafundisha njia yake.

Soma Zab 25

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 25:1-9