Zab 149
149
Sifa kwa Wema wa Mungu kwa Israeli
1 #
Isa 42:10
Haleluya.
Mwimbieni BWANA wimbo mpya,
Sifa zake katika kusanyiko la watauwa.
2 #
Ayu 35:10; Zek 9:9 Israeli na amfurahie Yeye aliyemfanya,
Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao.
3Na walisifu jina lake kwa kucheza,
Kwa matari na kinubi wamwimbie.
4 #
Mit 11:20
Kwa kuwa BWANA awaridhia watu wake,
Huwapamba wenye upole kwa wokovu.
5Watauwa na waushangilie utukufu,
Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.
6 #
Kum 7:1-2; Ebr 4:12; Ufu 1:16 Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao,
Na upanga mkali kuwili mikononi mwao.
7Ili kufanya kisasi juu ya mataifa,
Na adhabu juu ya kabila za watu.
8Wawafunge wafalme wao kwa minyororo,
Na wakuu wao kwa pingu za chuma.
9 #
Kum 7:1-2; Ufu 5:13; Rum 16:20; 1 Yoh 5:4 Kuwafanyia hukumu iliyoandikwa;
Hiyo ndiyo heshima ya watauwa wake wote.
Haleluya.
Iliyochaguliwa sasa
Zab 149: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.