Zab 114
114
Maajabu ya Mungu Wakati wa kutoka Misri
1 #
Kut 12:51
Haleluya.
Israeli alipotoka Misri,
Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni.
2Yuda ilikuwa patakatifu pake,
Israeli milki yake.
3 #
Kut 14:21; Yos 3:16 Bahari iliona ikakimbia,
Yordani ilirudishwa nyuma.
4 #
Zab 29:6; 68:16; Hab 3:6 Milima iliruka kama kondoo waume,
Vilima kama wana-kondoo.
5Ee bahari, una nini, ukimbie?
Yordani, urudi nyuma?
6Enyi milima, mruke kama kondoo waume?
Enyi vilima, kama wana-kondoo?
7Tetemeka, Ee nchi, mbele za uso wa Bwana,
Mbele za uso wa Mungu wa Yakobo.
8 #
Kut 17:1-7; Hes 20:2-13; Zab 107:35 Augeuza mwamba kuwa ziwa la maji,
Jiwe gumu kuwa chemchemi.
Iliyochaguliwa sasa
Zab 114: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.