Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 104:14-27

Zab 104:14-27 SUV

Huyameesha majani kwa makundi, Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu; Ili atoe chakula katika nchi, Na divai imfurahishe mtu moyo wake. Aung’aze uso wake kwa mafuta, Na mkate umburudishe mtu moyo wake. Miti ya BWANA nayo imeshiba, Mierezi ya Lebanoni aliyoipanda. Ndimo ndege wafanyamo vitundu vyao, Na korongo, misunobari ni nyumba yake. Milima mirefu ndiko waliko mbuzi wa mwitu, Na magenge ni kimbilio la wibari. Aliufanya mwezi kwa ajili ya nyakati, Jua latambua kuchwa kwake. Wewe hufanya giza, kukawa usiku, Ndipo atambaapo kila mnyama wa mwitu. Wana-simba hunguruma wakitaka mawindo, Ili kutafuta chakula chao kwa Mungu. Jua lachomoza, wanakwenda zao, Na kujilaza mapangoni mwao. Mwanadamu atoka kwenda zake kazini, Na kwenye utumishi wake mpaka jioni. Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. Dunia imejaa mali zako. Bahari iko kule, kubwa na upana, Ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika, Viumbe hai vidogo kwa vikubwa. Ndimo zipitamo merikebu, Ndimo alimo lewiathani uliyemwumba acheze humo. Hao wote wanakungoja Wewe, Uwape chakula chao kwa wakati wake.

Soma Zab 104