Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 31:20-31

Mit 31:20-31 SUV

Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake. Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu. Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani. Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi. Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi. Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao. Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu. Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema, Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote. Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa. Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.