Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 31:13-22

Mit 31:13-22 SUV

Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo. Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali. Tena huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao. Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu. Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu. Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku. Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia. Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake. Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu. Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.

Soma Mit 31

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mit 31:13-22