Mit 2:1-8
Mit 2:1-8 SUV
Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba maagizo yangu; Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu; Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu; Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika; Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA, Na kupata kumjua Mungu. Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu; Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili; Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu; Apate kuyalinda mapito ya hukumu, Na kuhifadhi njia ya watakatifu wake.