Oba UTANGULIZI
UTANGULIZI
Maana ya jina Obadia katika lugha ya Kiebrania ni “mtumishi wa BWANA” au “mwabudu BWANA”. Kitabu hiki hakitaji kiliandikwa lini, aidha mwandishi alipoishi sio yakini na mambo kadhaa ya ujumbe wake yanasimuliwa katika vitabu vingine vya manabii.
Ujumbe wa Obadia unahusu taifa la Edomu. Edomu maana yake ni “nyekundu” nalo ni jina aliloitwa Esau, wazao wake na nchi walimoishi (Mwa 36:1, 8-9; 25:15, 30). Kwa kuwa Israeli ilitawala Edomu baadaye Waedomi wakajikomba kulikuweko kutoelewana hata uhasama. Yuda ilipotekwa, Yerusalemu ukabomolewa, wakazi wake wakachukuliwa mateka, Edomu walifurahi wakajiunga na adui ya Yuda kupora mali ya Yuda. Ujumbe wa nabii Obadia unaeleza hali ya uhasama na mafarakano yaliyokuwapo kati ya mataifa ndugu. Pia ukatoa hukumu ya Mungu kwa Edomu. “Siku ya BWANA” ni wakati ambapo taifa la Mungu litalipiza kisasi kwa Edomu.
Yaliyomo:
1. Mungu atashusha kiburi cha Edomu, Aya 1-4
2. Mungu ataangamiza nchi ya Edomu, Aya 5-9
3. Sababu za kuangamizwa Edomu, Aya 10-16
4. Israeli na Yuda wataimarishwa, Aya 17-21
Iliyochaguliwa sasa
Oba UTANGULIZI: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.