Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hes 33:8-14

Hes 33:8-14 SUV

Wakasafiri kutoka hapo mbele ya Hahirothi, wakapita katikati ya bahari na kuingia jangwani; kisha wakaenda safari ya siku tatu katika nyika ya Ethamu, wakapanga Mara. Wakasafiri kutoka Mara, wakafikilia Elimu; huko Elimu palikuwa na chemchemi za maji kumi na mbili, na mitende sabini; nao wakapanga hapo. Wakasafiri kutoka Elimu wakapanga karibu na Bahari ya Shamu. Wakasafiri kutoka Bahari ya Shamu, wakapanga katika nyika ya Sini. Wakasafiri kutoka nyika ya Sini, wakapanga Dofka. Wakasafiri kutoka Dofka, wakapanga Alushi. Wakasafiri kutoka Alushi, wakapanga Refidimu, ambapo hapakuwa na maji ya watu kunywa.

Soma Hes 33

Video for Hes 33:8-14