Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hes 29

29
Sadaka za Sikukuu ya Mabaragumu
1 # Law 23:24; Zab 89:15; Isa 27:13; Zek 9:14; Mk 16:15; 1 Kor 15:52; Ufu 8:6-13 Tena mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi, mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi; ni siku ya kupiga tarumbeta kwenu. 2Nanyi mtasongeza sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu ya kupendeza kwa BWANA; ng’ombe mume mdogo mmoja, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu saba; 3pamoja na sadaka yake ya unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu ya kumi tatu kwa ng’ombe, sehemu ya kumi mbili kwa kondoo mume, 4na sehemu ya kumi moja kwa kila mwana-kondoo katika wale wana-kondoo saba; 5na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu; 6#Hes 28:11; Kut 29:38; Law 6:9; Hes 28:3; Dan 12:11; Hes 15:11,12zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya kuandama mwezi, na sadaka yake ya unga, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kama ilivyo amri yake, kuwa harufu ya kupendeza, ni sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto.
Sadaka za Siku ya Upatanisho
7 # Law 16:29-34; 23:27; Ezr 8:21; Zab 35:13; Isa 58:5; Mt 5:4; Lk 13:3,4; 1 Kor 9:27; 2 Kor 7:9; Yak 4:9 Tena siku ya kumi ya huo mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu; nanyi mtazitesa nafsi zenu, msifanye kazi yo yote ya utumishi 8#Law 22:20; Hes 28:19; 29:8; Kum 15:21; 17:1lakini mtamsongezea BWANA sadaka ya kuteketezwa, kuwa harufu ya kupendeza; ng’ombe mume mdogo mmoja, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza saba; watakuwa wakamilifu kwenu; 9pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu ya kumi tatu kwa huyo ng’ombe, na sehemu ya kumi mbili kwa huyo kondoo, 10na sehemu ya kumi moja kwa kila mwana-kondoo katika wale wana-kondoo saba; 11#Law 16:3,5na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya dhambi ya upatanisho, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji.
Sadaka za Siku ya Vibanda
12 # Law 23:34; Kum 16:13-15; Kut 23:16; 34:22; Eze 45:25 Tena siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi, nanyi mtamfanyia BWANA sikukuu muda wa siku saba; 13#Ezr 3:4; Ebr 10:1-18; Dan 9:24; Ebr 7:18; 8:13nanyi mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka isongezwayo kwa moto, harufu ya kupendeza kwa BWANA; ng’ombe waume wadogo kumi na watatu, na kondoo waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza kumi na wanne; wote watakuwa wakamilifu; 14pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu ya kumi tatu kwa kila ng’ombe katika wale kumi na watatu na sehemu ya kumi mbili kwa kila kondoo katika hao kondoo waume wawili; 15na sehemu ya kumi moja kwa kila mwana-kondoo katika wale wana-kondoo kumi na wanne; 16na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji.
17Tena siku ya pili mtasongeza ng’ombe waume wadogo kumi na wawili, na kondoo waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza kumi na wanne wakamilifu; 18#Hes 15:12; 28:7,14; Law 2:1pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji kwa hao ng’ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama hesabu yao ilivyo, kwa kuandama hiyo amri; 19na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji.
20Tena siku ya tatu mtasongeza ng’ombe waume kumi na mmoja, na kondoo waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu kumi na wanne; 21pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa hao ng’ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama hesabu yao ilivyo, kwa kuiandama amri; 22na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji.
23Tena siku ya nne mtasongeza ng’ombe waume kumi, na kondoo waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu kumi na wanne; 24na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji kwa hao ng’ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama hesabu yao ilivyo, kwa kuiandama amri; 25na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji.
26 # Yn 1:29; Ebr 7:26; 1 Pet 1:19; Ufu 1:6-14 Tena siku ya tano mtasongeza ng’ombe waume kenda, na kondoo Waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu kumi na wanne; 27pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa hao ng’ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama hesabu yao ilivyo, kwa kuiandama amri; 28na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na hiyo sadaka yake ya unga na sadaka yake ya kinywaji.
29Tena siku ya sita mtasongeza ng’ombe waume wanane, na kondoo waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu kumi na wanne; 30pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa hao ng’ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama hesabu yao ilivyo, kwa kuiandama amri; 31na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na hiyo sadaka yake ya unga na sadaka yake ya kinywaji.
32Tena siku ya saba mtasongeza ng’ombe waume saba, na kondoo waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu kumi na wanne; 33pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa hao ng’ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama hesabu yao ilivyo, kwa kuiandama amri; 34na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na hiyo sadaka yake ya unga na sadaka yake ya kinywaji.
35 # Law 23:36; Zab 47:5,6; Isa 11:10; 54:1; 60:1; Mt 28:1; Yn 7:37; Ebr 1:3; 4:9; Ufu 7:9-17; 11:15; 21:1; 22:1 Tena siku ya nane mtakuwa na kusanyiko la makini sana; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi; 36lakini mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kusongezwa kwa moto, harufu ya kupendeza kwa BWANA; ng’ombe mume mmoja, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu saba; 37pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa huyo ng’ombe, na kwa huyo kondoo mume, na kwa wale wana-kondoo, kama hesabu yao ilivyo, kwa kuiandama amri; 38na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na hiyo sadaka yake ya unga na sadaka yake ya kinywaji.
39 # Law 23:2; 1 Nya 23:31; 2 Nya 31:3; Ezr 3:5; Neh 10:33; Isa 1:14; Law 7:11,16; 22:21; 23:38; Hes 6:21; 7:21; Kum 12:6; 1 Kor 10:31 Sadaka hizo mtamsongezea BWANA katika sikukuu zenu zilizoamriwa, zaidi ya nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, kuwa sadaka zenu za kuteketezwa, na sadaka zenu za unga, na sadaka zenu za vinywaji, na sadaka zenu za amani. 40#Kut 24:3; Kum 5:27-31; 33:4; Yn 1:17; 7:19; Mdo 7:37,38Naye Musa akawaambia wana wa Israeli vile vile kama hayo yote BWANA alivyomwagiza Musa.

Iliyochaguliwa sasa

Hes 29: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia