Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hes 20

20
Maji ya Meriba
1 # Hes 33:36; 26:59; Kut 15:20 Kisha wana wa Israeli, mkutano wote, wakaingia bara ya Sini, katika mwezi wa kwanza, watu wakakaa Kadeshi; Miriamu akafa huko, akazikwa huko. 2#Kut 17:1-7; 16:2,7-12; Hes 16:19,42; 21:5; 1 Kor 10:10Na hapo hapakuwa na maji kwa ule mkutano; wakajikusanya juu ya Musa na juu ya Haruni. 3#Hes 14:2; Kut 17:2; Hes 11:1,33; 14:37; 16:32,33,49; Omb 4:9Watu wakashindana na Musa, wakanena, wakisema, Ingalikuwa heri kama tungalikufa wakati ule ndugu zetu walipokufa mbele za BWANA! 4#Kut 5:21; 17:3; Hes 11:5; Zab 106:21; Mdo 7:35,40Mbona mmewaleta kusanyiko la BWANA hata jangwa hili ili tufe huku, sisi na wanyama wetu? 5Na mbona mmetupandisha kutoka Misri ili kutuleta hata mahali hapa pabaya? Si mahali pa mbegu, wala tini, wala mizabibu, wala makomamanga; wala hapana maji ya kunywa. 6#Hes 14:5Musa na Haruni wakatoka pale palipokuwa mkutano, wakaenda hata mlangoni pa hema ya kukutania, wakaanguka kifudifudi; utukufu wa BWANA ukawatokea. 7BWANA akasema na Musa, akinena, 8#Kut 17:5; Neh 9:15; Zab 78:15,16; Isa 43:20Twaa ile fimbo, ukawakusanye mkutano, wewe na Haruni ndugu yako, ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji yake, nawe utawatokezea maji katika mwamba, na hivyo utawanywesha maji mkutano na wanyama wao. 9#Hes 17:10Musa akaitwaa hiyo fimbo kutoka mbele za BWANA kama alivyomwamuru. 10#Zab 106:33Musa na Haruni wakawakusanya kusanyiko mbele ya mwamba, akawaambia, Sikieni sasa, enyi waasi; je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu? 11#Yak 1:20; Kut 17:6; Kum 8:15; 1 Kor 10:4Musa akainua mkono wake akaupiga ule mwamba kwa fimbo yake mara mbili; maji yakatoka mengi, mkutano wakanywa na wanyama wao pia. 12#Hes 27:14; Kum 3:26; Law 10:3; Eze 20:41; 36:23; 1 Pet 3:15BWANA akamwambia Musa na Haruni, Kwa kuwa hamkuniamini mimi, ili kunistahi mbele ya macho ya wana wa Israeli, basi kwa sababu hiyo, hamtawaingiza kusanyiko hili katika ile nchi niliyowapa. 13#Zab 95:8Maji haya ni maji ya Meriba; kwa sababu wana wa Israeli waliteta na BWANA, naye alijionyesha kuwa mtakatifu kati yao.
Njia ya Kupitia Edomu Yakataliwa
14 # Amu 11:16,17; Kum 23:7; Oba 1:10,12 Kisha Musa akatuma wajumbe kutoka Kadeshi wamwendee mfalme wa Edomu, na kusema, Ndugu yako Israeli asema, Wewe wazijua taabu zote zilizotupata; 15jinsi baba zetu walivyotelemkia Misri, nasi tulikaa Misri muda mwingi, nao Wamisri walitutenda vibaya sana, na baba zetu pia; 16#Kut 2:23; 3:7; Mdo 7:35tena tulipomlilia BWANA, akatusikiza sauti yetu, akamtuma malaika, na kututoa tutoke Misri; nasi tupo hapa Kadeshi, mji wa mpakani mwako mwa mwisho; 17#Hes 21:22tafadhali utupe ruhusa tupite katika nchi yako; hatutapita katika mashamba, wala katika mashamba ya mizabibu, wala hatutakunywa maji ya visimani; tutaifuata njia kuu ya mfalme, tusigeuke kwenda upande wa kuume, wala upande wa kushoto, hata tutakapopita mpaka wako. 18Edomu akamwambia, Hutapita katika nchi yangu, nisije nikakutokea kupigana nawe kwa upanga. 19#Kum 2:6,28Wana wa Israeli wakamwambia, Tutakwea kwa njia kuu; tena kama tukinywa maji yako, mimi na wanyama wangu wa mifugo, ndipo nitakulipa thamani yake; nipe ruhusa nipite kwa miguu yangu wala sitaki neno lingine lo lote. 20#Mwa 27:41; 32:6; Amu 11:17; Zab 120:7; Eze 35:5,11; Amo 1:11Akamwambia, Hutapita katika nchi yangu. Kisha Edomu akamtokea ili kupigana naye, na watu wengi, na kwa mkono wa nguvu. 21#Kum 2:27,29; Amu 11:18; Rum 12:18; Ebr 12:14Basi hivyo Edomu akakataa kumpa Israeli ruhusa kupita katika mipaka yake; kwa hivyo Israeli akageuka na kumwacha.
Kifo cha Haruni
22 # Hes 33:37; 21:4 Kisha wakasafiri kutoka Kadeshi; wana wa Israeli, mkutano mzima, wakafikilia mlima wa Hori. 23BWANA akanena na Musa na Haruni katika mlima wa Hori, karibu na mpaka wa nchi ya Edomu, akawaambia, 24#Mwa 25:8; Hes 27:13; Isa 57:1,2; Ebr 12:23Haruni atakusanywa awe pamoja na watu wake; kwa kuwa hataingia katika nchi niliyowapa wana wa Israeli, kwa sababu mliasi kinyume cha neno langu hapo penye maji ya Meriba. 25#Kum 32:50Uwatwae Haruni na mwanawe Eleazari uwalete juu ya mlima wa Hori; 26umvue Haruni mavazi yake, ukamvike Eleazari mwanawe mavazi hayo; kisha Haruni atakusanywa kwa watu wake, naye atakufa huko. 27Musa akafanya kama BWANA alivyomwagiza; wakakwea katika mlima wa Hori mbele ya macho ya mkutano wote. 28#Kut 29:29; Hes 33:38; Kum 10:6; Hes 23:10; Ayu 30:23; Mit 14:32; Hos 13:14; Ufu 14:13Kisha Musa akamvua Haruni mavazi yake, akamvika mwanawe Eleazari mavazi hayo; Haruni akafa huko katika kilele cha mlima; Musa na Eleazari wakatelemka mlimani. 29#Mwa 50:3,10; Kum 34:8Na mkutano wote ulipoona ya kuwa Haruni amekufa, wakamwombolea Haruni muda wa siku thelathini, maana, nyumba yote ya Israeli ikamwombolea.

Iliyochaguliwa sasa

Hes 20: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia