Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hes 12

12
Haruni na Miriamu Wamwonea Wivu Musa
1 # Kut 2:21 Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi. 2#Kut 15:20; Mik 6:4; Mwa 29:33; 2 Fal 19:4; Zab 94:9; Isa 37:4; Eze 35:12Wakasema, Je! Ni kweli BWANA amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? BWANA akasikia maneno yao. 3#Zab 147:6; 149:4; Mt 5:5; 21:5; 1 Tim 6:11; 2 Tim 2:25; 1 Pet 3:4Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi. 4#Zab 76:9BWANA akanena ghafula na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje. 5#Kut 34:5; 40:38; Hes 16:19BWANA akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili. 6#Mwa 46:2; Ayu 33:15; Lk 1:11,22; Mt 1:20Kisha akawaambia,
Sikizeni basi maneno yangu;
Akiwapo nabii kati yenu,
Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono,
Nitasema naye katika ndoto.
7 # Ebr 3:2,5; Zab 105:26 Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa;
Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote;
8 # Kut 33:11; Kum 34:10; 1 Kor 13:12; Kut 33:19; 2 Pet 2:10 Kwake nitanena mdomo kwa mdomo,
Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo;
Na umbo la BWANA yeye ataliona.
Mbona basi ninyi hamkuogopa
Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?
9Hasira za BWANA zikawaka juu yao; naye akaenda zake. 10#Kum 24:9; 2 Fal 5:27; 2 Nya 26:19Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma.
11 # 2 Sam 19:19 Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi. 12#Zab 88:4; Efe 2:1-5; Kol 2:13; 1 Tim 5:6Nakusihi, asiwe kama mmoja aliyekufa, ambaye nyama ya mwili wake nusu imelika hapo atokapo tumbo la mama yake. 13#Yak 5:16Musa akamlilia BWANA, akasema, Mpoze, Ee Mungu, nakusihi sana. 14#Hes 5:2-3; Ebr 12:9; Law 13:46; 14:8; 2 Nya 26:20,21BWANA akamwambia Musa, Je! Kama baba yake angalimtemea mate usoni tu, hangaliona aibu muda wa siku saba? Na afungwe nje ya kambi muda wa siku saba, kisha baada ya hayo ataletwa ndani tena. 15#Kum 24:9; 2 Nya 26:20Basi Miriamu alifungwa nje ya kambi muda wa siku saba; wala watu hawakusafiri hata Miriamu alipoletwa ndani tena. 16Baada ya hayo watu wakasafiri kutoka Haserothi, wakapanga kambi katika nyika ya Parani.

Iliyochaguliwa sasa

Hes 12: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha