Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Law 24

24
Taa Isiyozimika
1Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2#Kut 27:20; 39:37; Hes 8:2-4Waagize wana wa Israeli kwamba wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya ile nuru, ili hiyo taa iwake daima. 3Hapo nje ya pazia la ushahidi, ndani ya hema ya kukutania, Haruni ataitengeza tangu jioni hata asubuhi mbele za BWANA daima; ni amri ya milele katika vizazi vyenu. 4#Kut 31:8; 37:17-24Atazitengeza hizo taa katika kile kinara kilicho safi mbele za BWANA daima.
Mikate ya Hema Takatifu
5 # Kut 25:30; 40:24 Nawe utatwaa unga mwembamba, na kuoka mikate kumi na miwili ya huo unga; sehemu za kumi mbili za efa, zitakuwa katika mkate mmoja. 6#1 Fal 7:48; 2 Nya 4:19; Ebr 9:2Nawe iweke mistari miwili, mikate sita kwa kila mstari, juu ya hiyo meza safi, mbele za BWANA. 7Nawe utatia ubani safi juu ya kila mstari, ili uwe ukumbusho kwa hiyo mikate, sadaka ya kusongezwa kwa BWANA kwa moto. 8#Hes 4:7; 1 Nya 9:32; 2 Nya 2:4Kila siku ya Sabato ataipanga mbele za BWANA daima; ni kwa ajili ya wana wa Israeli, agano la milele. 9#Mt 12:4; Mk 2:26; Lk 6:4; 1 Sam 21:6; Kut 29:33; Law 8:3; 21:22Nayo itakuwa ya Haruni na wanawe; nao wataila katika mahali patakatifu; kwa sababu kwake ni takatifu sana katika sadaka zisongezwazo kwa BWANA kwa moto, kwa amri ya milele.
Kufuru na Adhabu yake
10Ikawa mwana wa mwanamke wa Kiisraeli, ambaye babaye alikuwa Mmisri, akatokea kati ya wana wa Israeli; na huyo mwana wa mwanamke wa Kiisraeli, na Mwisraeli mmoja, wakapigana pamoja ndani ya marago; 11#Ayu 1:5; 2:5,9; Isa 8:21; Kut 18:22kisha huyo mwana wa mwanamke wa Kiisraeli akalikufuru hilo Jina, na kuapiza; nao wakamleta kwa Musa. Na jina la mamaye alikuwa akiitwa Shelomithi, binti ya Dibri, wa kabila ya Dani. 12#Hes 15:34; Kut 18:15,16Nao wakamtia kifungoni, ili wapate kuambiwa neno litakalotoka kinywani pa BWANA.
13Na BWANA akasema na Musa, na kumwambia, 14#Kum 17:7Mtoe huyo aliyeapiza nje ya marago; na wale wote waliomsikia na waweke mikono yao kichwani mwake, kisha mkutano wote na wamwue kwa kumpiga kwa mawe. 15#Law 5:1; 9:13Nawe nena na wana wa Israeli na kuwaambia, Mtu awaye yote atakayemlaani Mungu wake atachukua dhambi yake. 16#1 Fal 21:10; Zab 74:10,18; Mt 12:31; Mk 3:28; Yak 2:7Na yeye atakayelikufuru jina la BWANA hakika atauawa; mkutano wote watamwua kwa kumpiga kwa mawe; kama ni mgeni, kama ni mzalia, hapo atakapolikufuru jina la BWANA atauawa. 17#Kut 21:12; Mwa 9:6; Hes 35:31; Kum 19:11; Mt 26:52; Ufu 13:10Na mtu ampigaye mtu hata akafa, lazima atauawa; 18na atakayempiga mnyama hata akafa atalipa; uhai kwa uhai. 19#Kut 21:24; Kum 19:21; Mt 5:38; 7:2Na mtu akimtia mwenziwe kilema; vile vile kama alivyofanya, naye atafanyiwa vivyo; 20#Kut 21:23-25; Kum 19:21; Mt 5:38jeraha kwa jeraha, jicho kwa jicho, jino kwa jino; vile vile kama alivyomtia mtu kilema, naye atalipwa vivyo. 21#Kut 21:33Na mtu amwuaye mnyama atalipa; na yeye atakayemwua binadamu atauawa. 22#Hes 15:16; Kut 12:49; Law 19:34; Kum 10:17,19Mtakuwa na sheria moja tu, kwa huyo aliye mgeni, na kwa mzalia; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. 23#Kum 13:9; 17:7Musa akanena na wana wa Israeli, nao wakamtoa huyo aliyeapiza nje ya marago, wakamwua kwa kumpiga kwa mawe. Wana wa Israeli wakafanya kama BWANA alivyomwagiza Musa.

Iliyochaguliwa sasa

Law 24: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha