Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Omb UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kitabu cha Maombolezo ni mkusanyo wa tenzi tano zilizotungwa kuombolezea kuangamizwa kwa Yerusalemu na mateso yaliyotokana na maafa hayo, mwaka 587 Kabla ya Kristo Kuzaliwa. Hivyo jina lake latokana na yaliyomo. Ijapokuwa kitabu hakitaji jina la mwandishi wake, wengi husema kuwa ni nabii Yeremia (2 Nya 35:25), hata hivyo sio yakini.
Wayahudi walikuwa na tumaini kubwa la usalama juu ya mji Yerusalemu, Hekalu na utawala wa ukoo wa Daudi: Waliamini kuwa Mungu hawezi kuruhusu watu wengine kuharibu vitu hivyo. Ndio maana hawakukubali ujumbe wa nabii Yeremia kuhusu kutekwa na kuharibiwa Yerusalemu, Hekalu na ufalme wao. Baadaye walishuhudia unabii huo unatimilika (linganisha Yer 7:4-7 na Omb 2:6-7; Yer 18:18 na Omb 2:9-10; Yer 21:1-7 na Omb 4:20).
Ujumbe wa kitabu hiki ni kuwa Mungu uhukumu dhambi (1:8-9). Hasira ya Mungu kwa dhambi imefanya maangamizi yatokee kwa mji wao, Hekalu, ufalme wao na watu wake wawe mikononi mwa adui wao (2). Ijapokuwa walisingizia wakale wao kuwa ndio sababisho la maafa na mateso yao (5:7) adhabu yao ni kwa ajili ya uasi wao wenyewe (1:18, Yer 13:22). Hata hivyo Mungu ni mwenye rehema na upendo kuna matumaini ya wokovu (3:31-33). Lihitajiwalo kwa watu wake ni toba (3:39-42; 55-58). Mungu atawaondoa adui na watesi (3:64-66).
Yaliyomo:
1. Yerusalemu yaomboleza, Sura 1:1-11
2. Sala ya watu wa Yerusalemu, Sura 1:12-22
3. Bwana ndiye ameadhibu Yerusalemu, Sura 2
4. Uchungu, toba na matumaini, Sura 3
5. Taifa laombolezea Yerusalemu na matumaini, Sura 4
6. Maombi ya kurehemewa, Sura 5

Iliyochaguliwa sasa

Omb UTANGULIZI: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia